GET /api/v0.1/hansard/entries/1625538/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1625538,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625538/?format=api",
"text_counter": 289,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kibwana",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Naunga Sen. Faki mkono kuwa bei ya Kenya Airways na Jambo jet ziweze kushuka chini na huduma zao pia ziwe bora zaidi. Tumeanza kuona kuwa Kenya Airways bado huwa lazima ndege ziwe zimechelewa. Kama unaondoka saa mbili, unajikuta unaondoka saa saba ya mchana. Kama unaondoka saa saba, utajikuta unaondoka jioni. Kwa hivyo, haina utaratibu wa saa zake ukamilifu wa kuweza kufanya kazi vizuri. Tunaomba Serikali iweze kusaidia Kenya Airways wawe na huduma bora na pia malipo ya ndege yapunguzwe"
}