GET /api/v0.1/hansard/entries/1625740/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1625740,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625740/?format=api",
"text_counter": 85,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": null,
"content": " Asante, Bw. Spika. Ninataka kumuuliza Waziri wa Maji, ni lini lile bwawa lililoko katika eneo Bunge la Ganze, linaloitwa Rare litakamilika ili liweze kuwasaidia wananchi walioko katika Ganze Constituency na Kilifi kwa ujumla. Hii ni kwa sababu, Bw. Waziri, unaelewa kwamba wakati fulani, Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. William Ruto alikuwa katika eneo Bunge la Ganze na akaenda Rare na akaliona bwawa hili. Aliahidi kwamba hili bwawa la maji la Rare litakamilishwa ili liweze kumaliza ukame ndani ya eneo Bunge la Ganze. Ni lini unapofikiria, kama Waziri wa Maji, utaweza kufanya hiyo kazi ambayo Mhe. Rais mwenyewe aliweza kuahidi watu wa Ganze katika Kaunti ya Kilifi?"
}