GET /api/v0.1/hansard/entries/1625800/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1625800,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625800/?format=api",
    "text_counter": 145,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Kumekuwa na msongamano sana kutoka Kengelani mpaka Mtwapa kwa sababu ya ujenzi wa barabara ya Mombasa- Malindi. Kwa hivyo, magari mengi hutumia barabara ya Links Road iliyo Nyali ili waweze kutokea Bamburi-Nyali Centre wanapoelekea Kilifi na Malindi. Katika maeneo ya Quickmart, barabara hiyo imekuwa donda sugu kwa wakaazi wa Mombasa na Kilifi. Kukinyesha, magari husumbuka kupita pale kwa sababu ya vidimbwi vya maji ambavyo viko pale. Hii husababisha msongamano katika Links Road mpaka maeneo ya Shell Petrol Station. Je, hili tatizo litaisha lini? Kenya Urban Roads Authority (KURA) huandaa mkutano wa ushiriki wa uma na kesho yake, hao hukuja na kulaumu Kaunti ya Mombasa. Ikifika kesho kutwa, hao husema ya kwamba ni wawekezaji ambao wamejenga kando ya barabara ndio wanasababisha maji kutokwenda. Jambo lingine ningependa kuongelea ni taa ambazo ziko katika barabara ya Causeway. Hizo taa zinaleta aibu kwa Mombasa. Hii ni kwa sababu mtalii akishuka katika uwanja wa kimataifa wa Moi, anaona mataa lakini akianza kuingia mjini, anakaribishwa na giza. Watalii ambao wanaingia Mombasa kwa mara ya kwanza huwa wanajiuliza kama wanaingia kwenye mji ama msitu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}