GET /api/v0.1/hansard/entries/1625830/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1625830,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625830/?format=api",
    "text_counter": 175,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": null,
    "content": " Bw. Waziri, uwanja huu wa ndege wa Malindi ni wa zamani sana. Ulikuwapo zamani kabla Kisumu Airport haijajengwa. Natumai hata wewe umejionea wakati unatembea Malindi kwa likizo ama mapumziko. Kitu cha kushangaza ni kwamba mpaka saa hivi, hata kama kiwanja kina itwa Malindi International Aiport, kiwanja kile hakiko katika kiwango cha uwanja wa ndege wa kimataifa. Haya yote yametokana kwa kuwa wizara yako aidha imesusia, imekataa ama haifanyi juhudi zozote kuona ya kwamba wale waekezaji kama akina Flavio Briatore ambao walikuwa tayari kupanua kiwanja hicho katika mikadirio ya wizara yako na wale walioko tayari kutoka Italy. Nataka kujua ni kwa sababu gani Wizara yako, kufikia hivi sasa imewakataa hawa wawekezaji kupanua hiki kiwanja. Vile vile, nataka kukueleza ya kwamba hata ikiwa ni wakati wowote kuanzia hivi sasa, kunahitajika kupanuliwa kiwanja cha Malindi, wapo wawekezaji ambao wamejitolea. Wako tayari kutengeneza hicho kiwanja; mmoja wao ni yule ambaye nimekueleza hivi sasa. Wako tayari kukitengeneza kiwanja hicho kiwe kiwango cha kimataifa. Je, unaweza kueleza ya kwamba hawa wawekezaji wameweza kufanya mikakati ama ushirikiano gani na Serikali ama wizara yako ili kuona ya kwamba kiwanja hiki kimeweza kupanunuliwa kikawa katika status ya Moi International Airport ama Kisumu International Airport? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}