GET /api/v0.1/hansard/entries/162590/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 162590,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/162590/?format=api",
    "text_counter": 575,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kuipongeza Kamati ya Bunge inayohusika na masuala ya ukulima kwa kuwasilisha Ripoti mbele ya Bunge hili ili ijadiliwe. Tangu Mwenyekiti mpya, Bw. Mututho, achukue usukani katika Kamati hiyo, tunatarajia kuwa mambo mengi yatatokea. Tutaweza kuelewa sana mambo ya kilimo katika taifa la Kenya. Lazima tukumbuke kwamba kilimo ndicho uti wa mgongo wa taifa la Kenya. Sekta ya kilimo imekumbwa na matatizo mengi. Katika sekta hii ya pareto, itakumbukwa kwamba wakulima wengi waliweza kuangamia na kufutilia mbali kilimo cha pareto katika taifa la Kenya. Katika miaka ya tisini, Kenya ilikuwa katika orodha ya kumi bora katika Afrika, na dunia kwa jumla, miongoni mwa mataifa yanayokuza pareto kwa asilimia ya juu. Lakini sasa, tukipitia Ripoti ambayo imetolewa hapa Bungeni, tumegundua matatizo yanayoikumba sekta hiyo. Mojawapo ya matatizo hayo ni usimamizi mbaya, hali ambayo ililetwa na wale walioteuliwa."
}