GET /api/v0.1/hansard/entries/162592/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 162592,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/162592/?format=api",
    "text_counter": 577,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, Ripoti hii inaonyesha kwamba wakulima walitia bidii ya jino na ukucha na kutoa jasho yao ili waweze kupata mlo. Waliweza kuwasilisha pareto yao katika mwaka wa 2002, lakini walilipwa baada ya miaka mitatu au minne. Jambo hilo limewafanya wakulima wengi sana kuingiliwa na upweke. Vile vile, hadi sasa, wakulima waliopeleka pareto yao hawajalipwa. Huo ni ufisadi wa hali ya juu! Katika Bajeti ya Serikali kila mwaka, kuna pesa ambazo huwekwa katika sekta hiyo. Lakini haijulikani ni nani hulipwa pesa hizo! Kwa hivyo, wakulima wamekuwa samaki wadogo, huku samaki wakubwa wanaosimamia kampuni hiyo wakila!"
}