GET /api/v0.1/hansard/entries/1626148/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1626148,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626148/?format=api",
"text_counter": 120,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika, asante sana kwa kunipa fursa hii nichangie Ripoti hii ya Uwiano kuhusiana na sheria ya Kamari. Jambo la kwanza ni kuwa ijapokuwa Kamati hizi mbili zilikaa pamoja na kujaribu kuangalia yale masuala ya sheria ya kamari, kamari sio biashara. Kamari ni kamari. Kamari ina madhara mengi ikiwemo ile tunaita uraibu. Vilevile inasababisha athari za akili yaani mental health . Wengi wale ambao wanakwenda katika shuguli hizi, wanaathirika kiakili. Bila ya kwenda kwenye mchezo wa kamari, mtu yule anakuwa sio wa kawaida. Tatizo nililonalo na sheria hii ni kwamba imetoa fursa ya kufanya hata watu wadogo waweze kucheza kamari. Ikiwa kiwango cha pesa ambazo unaweza kutumia kwa kamari kimepunguzwa kutoka shilingi ishirini mpaka shilingi moja ina maana kwamba, kila mtu anaweza kuhiriki katika mchezo wa kamari. Bw. Spika, sheria nyingine ni kwamba, ndani ya vituo vyetu vya redio kwa sasa, matangazo mengi ni ya kamari. Kwa kipindi cha muda wa saa moja katika redio zetu za FM, wanatumia kutangaza kamari. Utasikia ukilipa shilingi mia, utapata shilingi elfu mbili au laki mbili. Imekuwa sasa ni jambo la kawaida katika nchi yetu kwamba, watu wanashiriki masuala ya kamari. Hili sio jambo nzuri kwa sababu, baadhi ya zile athari nilizotaja hapa, zitawahasibu Wakenya wengi na nchi haitapata watu wanaweza kufanya kazi ili kujenga nchi. Ningependekeza sheria ingefanywa ngumu au kali zaidi kuhusiana na wale wanakiuka sheria kuhusiana na masuala ya kamari. Kwa mfano, hivi vituo vya redio vinavyotangaza mara kwa mara masuala ya kamari, vingepunguziwa muda wanatakikana The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}