GET /api/v0.1/hansard/entries/1626149/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1626149,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626149/?format=api",
"text_counter": 121,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kutangaza kamari. Bila kufanya hivyo, ina maana kila mtu ataingia katika mchezo wa kamari na si vizuri kwa nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo, Shirika la Communications Authority of Kenya (CAK) lazima liwe macho ili kuhakikisha zile kamari zinatangazwa mara kwa mara na zinazoadhiri watu wetu zinapunguzwa. Bw. Spika, kwa sababu ya hii kamari iko katika vyombo vya habari na kila mahali, hata zile kasino ambazo zamani zilikuwa sehemu za kamari, hivi sasa zimefifia na biashara nyingi za kasino zimefungwa. Hii ni kwa sababu wengi wanashiriki katika kamari ambayo iko kwa mitandao, yaani online, na zile sehemu ambazo kamari ilikuwa ikichezwa zamani, zimebadilika na zikawa hata mahali pa kuishi. Watu wanacheza kamari. Bibi na bwana wanashiriki katika kamari na kila moja akijaribu kushabikia timu yake ya mpira ama jambo fulani ambalo iwapo atashinda, watapata zile pesa wamewekeza katika kamari hiyo. Kwa hayo mengi, Bw. Spika, ninapinga Mswada huu."
}