GET /api/v0.1/hansard/entries/1626428/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1626428,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626428/?format=api",
    "text_counter": 104,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "elimu zilikuwa za chini sana. Wakenya wengi katika maeneo yale hawakubahatika hata kwenda shule ama kupata huduma za afya kama Wakenya wengine. Uanzilishi wa hazina hii ulikuwa na malengo mazuri sana. Lakini baada tu kuanzishwa, kukaingia mambo mengi ya kusikitisha ambayo yamesababisha kwamba mpaka sasa hazina hii haijatumika kikamilifu. Kwa mfano, baada ya kuanzishwa ilichukua muda mrefu sana kuweza kupata kanuni ama sheria endelezi, delegatedlegislation ama regulations za kuweza kuendesha hazina hii. Za kwanza zilipotengenezwa zilipatikana ziko na makosa kwa sababu hawakuhusisha Council of Governors (CoG) ama kaunti zetu. Wao wakaenda mahakamani wakazibatilisha; tukarudi tena na tukachukua muda mrefu katika Seneti ya Tatu ambapo tuliweza kupitisha kanuni hizo. Pia kupitishwa kwake, ilibidi tutumie mbinu fulani ambazo sitaweza kuzieleza - ili siweze kupita ndio wananchi wafaidike. Hii ni kwa sababu kulikuwa na watu - Maseneta katika Bunge hili, ambao walikuwa tayari kuzipinga ili zisitekelezwe. Kwa zaidi ya miaka minane baada ya hazina hii kuanzishwa, zile kaunti zilizokusudiwa kupata manufaa hazikuweza kupata manufaa yale. Wengi walikuwa wamepewa zabuni za kuanzisha kazi katika maeneo ya zile kaunti. Nakumbuka kuna watu kadhaa walinifuata wakati nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya DelegatedLegislation katika Bunge lililopita, wakitaka kujua kanuni zitapitishwa lini ili waweze kumaliza zile kazi walikuwa wameweza kufanya na walipwe pesa zao ambazo walikuwa wanadai ile hazina. Baada ya kupitisha kanuni, vile vile, ilifika wakati wa kuamua zile kaunti ambazo zitafaidika katika awamu ya pili - ndio hapo sasa kaunti zikaongezeka hadi 34 badala ya zile 14 za kwanza. Kukaongezeka kaunti zingine 20 ambazo pia wao walidai kwamba wametengwa; ikiwemo Kiambu ambapo kuna matajiri upande moja na maskini upande mwingine. Pia ilipatikana kuwa ni kaunti ambayo imetengwa. Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba Serikali mpaka hivi sasa, pesa ambazo zimetengwa kwa hazina hii kwa miaka yote ambayo imepita ni Kshs56 bilioni. Katika hizi, ni asilimia 20 ambazo mpaka sasa zimeweza kutoka katika hazina kuu kwenda katika maeneo hayo. Hii ni kwa sababu sasa, sio kaunti, ni maeneo ambayo yametengwa. Tulitoka katika kaunti, sasa tuko katika maeneo. Kwa hivyo, ijapokuwa malengo ya hazina hii yalikuwa ni mazuri sana, lakini utepetevu katika Serikali umefanya kwamba hazina hii isiweze kutumika kikamilifu. Wakati tunaelekea mwisho wa hazina hii, kwa sababu hii hazina ina kiwango cha miaka 20 - tayari zaidi ya miaka 15 yamepita - kuna hatari kwamba yale malengo ambayo yalikuwa yamewekwa na hazina hayataweza kufikiwa. Vile vile, maeneo mengi pia yanaendelea kutengwa. Ijapokuwa tuna Serikali za kaunti, kuna maeneo mengi katika kaunti zetu ambayo yanatengwa kwa sababu ya siasa. Kama Mbunge wa eneo lako haelewani na gavana, ina maana kwamba eneo lako halitapata maendeleo na baada ya miaka mitano litakuwa limetengwa kuliko yale ambayo yalitengwa kutoka wakati wa Uhuru mpaka hivi sasa. Jambo lingine pia la kusikitisha ni kwamba wakati tulipokuwa tunapokea maoni ya washikadau kuhusiana na Mswada huu wa hazina ya usawa; yaani Equalisation Fung, kulikuwa na maoni kutoka kwa ndugu zetu hapa Nairobi, maeneo ya Pumwani, ambao The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}