GET /api/v0.1/hansard/entries/1626429/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1626429,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626429/?format=api",
"text_counter": 105,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "walisema, sisi pia tunataka tujumuishwe na yale maeneo yametengwa kwa sababu kwa miaka mingi hapa Pumwani, hapa Nairobi, kama kilomita nne kutoka hapa Bungeni; tumekaa hapo, hatuna maji ya mfereji, huduma za afya za kisawasawa, huduma za usafi, yaani sanitation na mambo kama hayo. Na kwamba wao pia wamesema kwamba, sisi pia twahitaji kupewa pesa kutoka kwa hazina hii ili tuweze kuboresha mazingira na maeneo yetu ambayo tunaishi. Kwa hivyo, nina imani kwamba itakapofika wakati wa kujadili awamu ya tatu ya mwelekeo wa kugawanya hazina hii, ninafikiri kaunti zote 47 zitakuwa zimeingia katika mfumo kwamba zote zimetengwa. Tunapopitisha sheria hii, lazima tuangalie ni njia gani ambayo tutasukuma Serikali ili zile fedha ambazo zinatengwa katika hazina hii zinaweza kutumika kwa njia ambayo itasaidia wale ambao wanakusudiwa kutumikia. Suala lingine ni kwamba kuna mgongano baina ya Serikali za kaunti na mashirika ambayo yanatoka kwa Serikali kuu yanayosimamia hazina hii. Kwa mfano, pesa zile ambazo zinasimamia miradi ya maji, kule pwani katika maeneo ya Kwale, Kilifi na Lamu, zinakwenda kwa Coast Water Services Board. Ijapokuwa sisi tunashiriki na hii sheria imetoka katika Bunge hili, sisi kama Seneti hatuna uwezo wa kufanya audit ya fedha zile. Hii ni kwa sababu audit yao, kwa vile imepitia kwa mashirika ya Serikali Kuu, inakwenda katika National Assembly. Kuna fedha zingine ambazo zinaingia katika Serikali zetu za kaunti kusimamia miradi kama hiyo. Kwa mfano, miradi ya barabara yanafanywa na Serikali za kaunti. Kwa hivyo, huu mgongano inakuwa shida kuweza kukagua au kusimamia fedha hizi na kuhakikisha kwamba zinafanya yale mambo ambayo yamenuia kufanya. Wengi ambao wanafanya kazi hizi labda ni Wabunge, Maseneta na kwa hivyo inakuwa tatizo kusimamia ukaguzi ama audit ya fedha hizi ili kuona kwamba zile kazi ambazo zinanuiwa kufanywa zinafanyika ili tuweze kutoka katika lile lindi la kutengwa na wao waweze kupata huduma kama vile sehemu zingine za nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo, ninaunga mkono Mswada huu. Lazima tuhakikishe kwamba zile fedha zinazotengwa kila mwaka kwa hazina hii; kwanza zinawekwa kwenye sheria,"
}