GET /api/v0.1/hansard/entries/1626472/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1626472,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626472/?format=api",
    "text_counter": 148,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa hii fursa umenipa, kuunga mkono Mswada huu wa usawazishaji wa maeneo ya magatuzi, almaarufu Equalization Fund. Mhe. Spika wa Muda, naunga mkono shingo upande kwa sababu yale maeneo 14 ambayo yalitarajiwa yafaidike na hizi fedha yalipanuliwa mpaka yakawa maeneo 34. Historia ya Kenya iko bado bayana ya kwamba tulipopata Uhuru, kuna sera iliyoandikwa na aliyekuwa Waziri wa Mipango ya Maendeleo, Mhe. Tom Mboya, inaitwa Sessional Paper No.10 of 1965, ilyosema kwamba tumepata Uhuru na saa hii tunajitawala wenyewe, je fedha zetu tutazisambaza namna gani ili Kenya yetu iendelee? Fedha nyingi zilipelekwa maeneo ambayo yana mvua nyingi, na rotuba ya juu, kwa kimombo, highpotential areas . Haya maeneo yalikuwa Mlima Kenya, Bonde la Ufa, Magharibi na Nyanza. Maeneo ya Pwani, Lower Eastern na Northern Frontier District yaliachwa nyuma kimaendeleo kwa sababu rotuba ya huko ilikuwa kidogo na pia mvua ilikuwa chini sana. Bi. Spika wa Muda, wakati wa kuandika Katiba mpya, waandishi wa Katiba wakasema tuache Ibara ya 204 ili tutenge fedha chache za kusawazisha maeneo ambayo yaliachwa nyuma kimaendeleo kwa sababu ya ile sera ya waka 1965 ama Sessional Paper No.10. Jambo la kushangaza ni kwamba Bunge hili liliunga mkono kuongeza yale maeneo ambayo yangefaidika. Kati ya zile kaunti 14 zinazofaa kufaidika na fedha za usawazishaji wa maeneo yaliyoachwa nyuma kimaendeleo, Taita Taveta ilikuwa mojawapo. Kwa zile fedha za kwanza zilizokuja kwa magatuzi hayo, Taita Taveta ilitumia kutoa maji kutoka laini ya kwanza ya Mzima na maeneo kama Mbulia na Mbololo yakapata maji. Wakati sera hii ilibadilishwa ama sera ya pili kuchapishwa, Taita Taveta imebakia na maeneo mawili peke yake. Moja ni kata ndogo kule Kasighau, ambayo huu mwaka inapata Shilingi 10,300,000. Kuna maeneo mengine ya Taveta, kata ndogo ya Challa, ambayo inapata Shilingi 11,000,000. Kuna swali nauliza kila siku. Wakati tulisema Kaunti ya Taita Taveta haina maji kwa sababu zile pesa zilikuwa zitekeleze miradi ya maji, je, inaonyesha ya kwamba The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}