GET /api/v0.1/hansard/entries/1626473/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1626473,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626473/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "maeneo yote yalipata maji? Zile changamoto zilizokuwa zinakumba maeneo mengi ya Taita Taveta kama ukosefu wa maji mpaka leo zipo. Wakati kata ndogo kama Kasighau inapewa Shilingi 11,000,000 ya kutekeleza miradi ya maji, hapo kando kuna maeneo ya Marungu ambayo pia ni kame sana. Hapo karibu kuna maeneo ya Sagala ambayo pia ni kame sana. Ukiangalia kata ndogo ya kule Taveta kama Challa wanapopewa Shilingi 10 milioni za kufanya mradi wa maji, hapo kando kuna wadi ya Mahoho na Mata ambazo hazina maji. Vigezo vilivyotumika katika utafiti na hii Tume ya Commission on Revenue Allocation (CRA) kubaini ni maeneo gani yatakayopata fedha vilikuwa vya aina gani? Kando na maji, fedha hizi zilifaa kutengenezeza barabara. Tangu tupate Uhuru, barabara ambazo zimetengenezwa ni za vichochoroni. Kuna barabara zinaitwa International Trunk Roads, kama hii ya Voi kwenda Taveta. Ile ni barabara inayounganisha nchi mbili. Barabara nyingine iliyotengenezwa Taita Taveta kando na hiyo ni ya kutoka Mwatate kwenda Wundanyi. Barabara nyingine iliyotengenezwa ni kilomita sita ya Bura Mission kwenda Bura Station. Barabara zingine zote, tingatinga huwa zinakuja kufungua mradi halafu zinakimbia. Barabara hizo zinachukua miaka na mikaka kutengenezwa. Kwa mfano, barabara ya Bura-Mughange-Werugha-Wundanyi-Mtoa Magoti, tangu izinduliwe mwaka 2020 mpaka leo, haijaisha ilhali inahitaji Shilingi 2 bilioni peke yake. Bi. Spika wa Muda, tulitazamia ya kwamba tukipata hizi pesa za kusawazisha maeneo ya Kenya, tungezitumia kutengeneza barabara zetu sisi wenyewe. Aliyekuwa Waziri Mkuu, Mhe. Raila Odinga, siku moja alitumia barabara ya Bura-Mghange- Werugha. Ile barabara ilikuwa mbaya na akasema ni kama ya kuenda jehanamu. Nashukuru kwani mwaka 2020 wakati tulienda kule Ikulu kupigania fedha za Division on Revenue Allocation (DORA), alimwomba Mhe. Rais Uhuru tutengenezewe ile barabara na Mhe. Rais akakubali ingawaje kutekelezwa kwa mradi huo kumekuwa kwa shida. Barabara nyingi za Kaunti ya Taita Taveta ni mbaya. Kama tungegawigwa zile pesa za usawazishaji, tungefanya hiyo miradi ya kuboresha barabara zetu. Taita Taveta ni eneo ambalo udongo wake uko na rotuba nyingi lakini shida ni maji. Iwapo Kenya inataka kuongeza utajiri kupitia kuuza bidhaa ng’ambo, basi, tungeangazia ile milioni moja ya mashamba ya Taita Taveta ya range land . Tungetumia hela hizo kulisha ng’ombe na mifugo na kuuza ng’ambo kwa kuwekeza tu kwa miradi ya maji. Challa, Njoro na Mzima kuna maji mengi. Tungefanyiwa mradi wa kuleta maji ili yatumike kwa ukulima wa unyunyiziaji wa mashamba, tungekuwa na nyasi nyingi za kuuza mpaka ulaya, lakini miradi hiyo haijafanyika. Fedha kama hizi za kusawazisha maeneo mbalimbali ya Kenya ni muhimu kufanya miradi kama hiyo. Bi. Spika wa Muda, Taita Taveta ina maji mengi sana. Kuna Mzima II ambayo inasambaza maji kuanzia Kaunti ya Taita Taveta, Kwale, Kilifi hadi Mombasa. Tungepata fedha kama hizi, tungezitumia kufanya miradi kama hiyo. Jambo la kushangaza ni kwamba baada ya mradi wa Mzima II kutotekelezwa, leo hii tunasikia kuna mabwenyenye, watu wasioeleweka, wamechukua maji Kutoka Mzima II kwa kutumia Line 1 ya Kenya Pipeline Corporation (KPC). Sijui wanayatumia kufanya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}