GET /api/v0.1/hansard/entries/1626474/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1626474,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626474/?format=api",
    "text_counter": 150,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "nini, lakini ni jambo la kuhuzunisha. Ni jambo la kuudhi kwamba tunaweza kutoa maji Taita Taveta kupatia watu wengine, ilhali watu wa Taita Taveta hawana maji. Kaunti ya Taita Taveta imewachwa kimakosa kwa hizi pesa za usawazishaji wa maeneo kiuchumi. Nikiangalia majirani wetu wote, kuanzia na jirani wa kwanza, Kaunti ya Kilifi, inapata Shilingi 878,000,000. Jirani mwengine ni Kaunti ya Kitui ambayo inapata Shilingi 646,000,000. Jirani mwengine ni Kaunti ya Kwale, ambayo inapata Shilingi 475,000,000. Eneo Bunge moja la Kinango, ambalo tumepakana upande wa Macknon Road, linapata Shilingi 265,000,000. Kaunti ya Kajiado pia ni jirani yetu na inapata Shilingi 674,000,000. Kaunti ya Tana River ambao pia ni jirani yetu inapata Shilingi 719,000,000. Ninachojiuliza ni: Je, ni vigezo gani vinavyoonyesha kwamba Kaunti ya Taita Taveta haihitaji pesa za kusawazisha maeneo yaliyoachwa nyuma kimaendeleo hadi inapewa Shilingi 21,000,000 pekee? Hilo ni jambo la kutamausha, kuudhi na kufisha moyo. Watu wa Taita Taveta hawajisikii kama wako Kenya. Nafikiri ni kwa sababu ni watu wachache mno, ndio maana watu wanaona kwamba hawafai sababu kura yao siyo nyingi. Wakati wa kupeana pesa za kusawazisha maeneo yaliyowachwa nyuma kimaendeleo, wakaona hawafai maana hawana kura. Kando na kuwa tuko wachache, hatuna maji, barabara na vituo vya afya wala stima. Kero la wanyama pori ni kitu kingine ambacho Serikali ya Kenya imekataa kuangazia kabisa. Hao watu wameachwa nyuma kimaendeleo, hawana mtetezi, hawajui watajisaidia namna gani na katika bidii yao ya kulima, kufuga mifugo kama mbuzi, ng’ombe na kondoo, Wanyama pori kama simba na chui wanawala wanyama wao. Ndovu wanamaliza chakula chao. Kama kungekuwa na njia, kule Taita Taveta - sisi tunapakana na Tanzania – tukatiwe eneo letu twende Tanzania. Hii ni kwa sababu haifai tena, haina maana tena kusikia kwamba sisi ni Wakenya lakini yale madhila na shida tunazopata kama Wakenya ziko vile zilivyo."
}