GET /api/v0.1/hansard/entries/1626489/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1626489,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626489/?format=api",
"text_counter": 165,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninaomba mheshimiwa yeyote anaponyanyuka kutoa hoja, ajue kwamba Mkenya yeyote popote alipo anaposikiza, lazima tumpe moyo na sababu ya kujivunia kuwa Mkenya, japo fedha hazitoshi, lakini waone kuna jambo nzuri linatendeka katika Serikali ya Kenya. Lisilokuhusu, usiliandame. Sisi watu wa Bungoma tunashukuru kidogo tumepata lakini tunasema tunahitaji fedha zaidi. Wanapogawa muda mwingine, tunataka ipande kutoka Shilingi 95 milioni ije kama bilioni, jinsi kaunti zingine zinapata. Hii ni kwa sababu ukiangalia mgao wa fedha, jinsi tulivyopitisha hapo awali, baadhi ya kaunti ambazo zinapata fedha nyingi hata sasa, katika bajeti bado wanapata fedha nyingi na kwa muda mrefu wamekuwa wanapata hizi fedha. Lazima tufuatilie tujue, miradi gani inatekelezwa na serikali za kaunti; wanahusisha wananchi katika utekelezaji wa miradi na iwapo miradi hii inaafiki matarajio ya wapiga kura ama wanaoishi katika maeneo haya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}