GET /api/v0.1/hansard/entries/1626490/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1626490,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626490/?format=api",
"text_counter": 166,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninapoangalia Kaunti ya Busia ambayo ni jirani yetu kule, wamepewa Shilingi 29 milioni. Hizi pesa hazijakuja kimzaha. Kuna sababu ambayo imeshinikiza Serikali kuweka fedha katika Kaunti ya Busia. Haimaanishi kwamba Busia ilipokuwa na Naibu wa Rais na Mawaziri ama walipokuwa na Mhe. Amos Wako katika Serikali watu wa Busia walikuwa katika shamba la asali na nyama. Haiwezekani. Kuna changamoto watu hawa walikuwa nazo ndiposa fedha zimewekwa kwa bajeti vile vile kama Wakenya waweze kuimarisha maisha yao. Nashukuru wameweka Kaunti ya Trans Nzoia hapa. Wamepewa Shilingi 12 milioni japo kuna viongozi huko hawashukuru kwa chochote. Wanabwata tu, wanaongea tu. Lazima tutafuata tujue hizi fedha zinazoenda Trans Nzoia zinatumika kivipi katika eneo Bunge la Endebbes. Lazima tutawaeleza watu katika eneo Bunge hili na Trans Nzoia fedha za usawazishaji zinatumika vipi ili wajue kuwa Seneti linawajali; japo kuna wale wanapinga na kutusi Serikali na wakututusi sisi Maseneta, tutawapa pesa lakini tutafuata kuhakikisha hizo pesa zinafanya kazi. Zaidi ya hapo, wanakandarasi wanaofanya hizo kazi lazima watoke katika kaunti husika. Hii ni kwa sababu Haiwezekani Seneti tunapitisha fedha kama hizi na wale wanakandarasi ni watalii wa kibiashara. Wanatoka Nairobi na kaunti zingine kufanya kazi ambayo wananchi wa kaunti husika wanaweza kufanya."
}