GET /api/v0.1/hansard/entries/1626491/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1626491,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626491/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Ninaunga mkono kaunti hizi ambazo zimeorodheshwa hapa. Wale waliopewa pesa kidogo waongezewe, kama ndugu yangu wa Taita Taveta. Ana haki ya kudai pesa ziongezwe. Wale ambao wamekuwa wanapewa pesa nyingi na hatuoni matunda, wapunguziwe kwa sababu huenda hizi pesa zinaenda katika mifuko ya watu wachache ilhali wengi wanaumia. Hawana maji, barabara au madawa hospitalini. Hatuwezi kukubali mambo kama haya katika awamu hii ya Serikali."
}