GET /api/v0.1/hansard/entries/1626498/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1626498,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626498/?format=api",
    "text_counter": 174,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa ya kuchangia pesa za Hoja inayoendelea kuhusu marginalised communities, groups na makaunti. Kulingana na mimi Kamati ya Fedha na Bajeti walifanya kazi ya huzuni kwa kaunti zingine. Kenya tuna makaunti 47. Tukiwa hapa, hakuna Seneta mkubwa au mdogo. Hakuna kaunti ndogo au kubwa kwa sababu ikifika mambo ya keki ya Kenya mzima, kila mtu anafaa asherehekee. Wiki jana, tulikuwa tunapitisha mambo ya pesa zitakaoenda kule mashinani ya kaunti 47. Wakati mwingine utapata hii Kamati ya Fedha na Bajeti inatuletea ripoti tupitishe. Hizo ripoti siyo njia inayofaa sababu zitaleta mgawanyiko katika kaunti zingine na kwa sisi, Maseneta. Kwa sababu, pesa kama iko Kenya, hakuna kaunti yeyote haifai kupata hizi pesa. Tumeona kaunti zingine zinapata karibu Shilingi 1 bilioni, zingine Shilingi 50 milioni na zingine Shilingi 20 milioni. Bi. Spika wa Muda, hiyo inamaanisha hizi pesa za marginalised communities zinafaa kila kaunti ipate. Ninashindwa kwa nini Kaunti ya Embu haipati pesa na unapata kaunti ya Kitui, Meru na Tharaka Nithi zinapata pesa. Kaunti ya Embu iko na sub-county nne. Kuna sub-county ya Mbeere South ambayo ingepata pesa kuongezea bajeti inayopelekwa mashinani na gavana. Huko Mbeere South utapata kuna watu wanatembea kilomita 20 au 50 kwa sababu hakuna magari na barabara zimeharibika. Huko hakuna hata maji. Leo asubuhi tulikuwa na Mhe. Waziri wa Maji ambaye niliuliza Kaunti ya Embu itaangaliwa namna gani kuhusu mabwawa ya maji kama kaunti za Tharaka Nithi na Meru. Kuna mabwawa matatu kule Embu, Manyatta, Mbeere North na Runyejes. Tunauliza vile tutapata maji juu ya kilimo chetu ambacho ni muguka. Bajeti inakuja hapa halafu, unakuta kwamba, sisi hatuko kwa hii ripoti. Hakuna kitu Embu imepata. Mwaka jana, kwa hizi pesa za marginalised communities, Embu haikupata. Utapata miradi ya kilimo yanaenda chini kwa sababu ya kukosa maji. Pia miradi ya barabara na hospitali yako nyuma. Pia shule zina shida. Mambo haya yote ni ya kuhuzinisha sana. Yale mambo yanafanyika na watu wanaofanya kazi ya mgao wa pesa kama hizi hawafuatilii njia inayofaa. Kule Mbeere North na Mbeere South, kuna shida nyingi sana. Janga la njaa likija, linafuata Mbeere South na Mbeere North. Hizi pesa zinafaa ziende kusaidia wale watu wajisaidie. Bi. Spika wa Muda, ningetaka kuwaambia Kamati ya Fedha na Bajeti wamegawa hizi pesa kwa njia haileweki, ni njia iko na mapendeleo na iko na mrengo hauleweki. Wamefanya jambo la kuhuzunisha kama Embu haiko katika hazina hii ya uwasa wa mgao wa pesa. Ninakumbuka mwaka jana sikupitisha pesa hizi. Kama hii Kamati haitafanya yale yanayofaa, inafaa kutimuliwa na ivunjwe ili tupate ile Kamati itasaidia kaunti zote. Pesa zinakuja na zingine ni msaada kutoka nchi za ng’ambo au ni sisi tunalipa. Ni afadhali kila kaunti ipate pesa kulingana na vile inafaa. Kaunti nyingi za hizo"
}