GET /api/v0.1/hansard/entries/1626501/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1626501,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1626501/?format=api",
    "text_counter": 177,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "unapata hakuna kitu kaunti zingine zinafanya. Kaunti zinajaribu kutoka chini mpaka juu, unapata hazipewi pesa kulingana vile inafaa. Bi. Spika wa Muda, haya ni mambo ya kuhuzinisha sana. Utapata hoja italetwa Bunge na tuipinge kwa sababu italeta shida ya vyama na mambo mengine. Mambo kama haya yatafanya watu wakosane. Hata mwaka jana, nilisema sitaunga mkono, tuliambiwa tuandike barua kwa wale watu wanahusika na mgao wa pesa hizi. Niliongea na gavana na akaandika kila kitu. Lakini, siku ya leo, Kaunti ya Embu haikua kwa hii ripoti. Kuna kaunti 44 zile zimepata pesa. Ningeomba wakati mwingine, Embu iangaliwe na ipate pesa kutoka kwa hazina hii. Ningependa kusema, hata kama ni nani atakuja kuniambia niunge mkono hii, tukienda kupiga kura, hii nitapinga. Kwa hivyo, ninapinga huu Mswada."
}