GET /api/v0.1/hansard/entries/166467/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 166467,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/166467/?format=api",
"text_counter": 258,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Nashukuru Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Mswada huu. Mswada huu ni wa maana sana katika nchi yetu. Nimewasikia wenzangu wakizungumza kuhusu yaliyomo katika Mswada huu. Jambo la kushangaza ni kuwa wengine wanaamini kwmaba sisi Wakenya hatuwezi kujiamuria mambo haya. Ni lazima tutafute mtu kutoka nje ili asimamie maswala haya ya kisheria. Hii ni ndoto mbaya sana. Nchi hii imetumikiwa na majaji wakuu kwa miaka mingi. Wengi wao wakiwa ni Wazungu, Wahindi na pia ndugu zetu Wakenya. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba tumelalamika miaka nenda, miaka rudi kuhusu usimamizi mbaya wa mahakama zetu. Wakati tulikuwa na Jaji Mkuu Mkenya ulalamishi ulikuwepo. Wao wengine walipokuwepo, ulalamishi ulikuwepo. Je, shida yetu ni nini? Shida yetu ni kukosa kuchunguza tunapowaajiri majaji hao au ni sisi Wakenya ambao hatutaki kutii sheria za nchi hii? Ukiangalia bodi ambayo tunataka kuunda hapa, kuna mapendekezo tuwe na watu kutoka nje. Kuna mhe. Mbunge mmoja ambaye amesema tunaweza kupata wataalam wa sheria kutoka nchi ya Somalia na kuwateua katika bodi hii. Kama tunavyojua, Somalia haina mahakama wala Serikali. Je, watu wa nchi hiyo wataongoza vipi mahakama zetu? Bw. Naibu Spika wa Muda, tumesomesha watu wetu sana na tunaendelea kulipa karo kwa watoto wetu. Kwa mfano, katika eneo langu, asilimia 60 za pesa tunazopata hugharamia elimu ya watoto wetu. Jambo ambalo linanifanya nitilie mkazo mambo ya elimu ni kwa sababu taifa hili linahitaji watu ambao wamesoma sana. Ni watu hawa ambao watasimamia nyadhifa mbalimbali katika Serikali yetu na uchumi wetu. Tunapozungumza hapa Bungeni, sisi kama viongozi, ni lazima tujue ya kwamba tuna wataalam wengi wa maswala ya kisheria katika nchi hii. Kwa hivyo, hatutaki wataalam kutoka nje kuja kusimamia bodi na mahakama zetu. Watu hao watachunguzaje watu wetu? Mtu ambaye hatumjui amezaliwa wapi na hatujui tabia na elimu yake atafanya kazi vipi?. Je, yeye atawezaje kuwachunguza watu wetu? Pengine watu hawa wameiba katika mataifa yao na kuhusika ma maovu mengine. Itakuwa ni aibu kwa watu wetu kuchunguzwa na watu kutoka nje. Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumewanyima watu wetu haki na usawa. Bw. Naibu Spika wa Muda, ni lazima tuwaamini watu wetu. Wakenya wamehitimu katika nyanja mbalimbali. Huku nje wanatuchekelea tukipendekeza wafanyiwe uchunguzi na watu wa kutoka nje. Kwa nini hatutaki watu wetu kufanya kazi hii?"
}