GET /api/v0.1/hansard/entries/166468/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 166468,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/166468/?format=api",
    "text_counter": 259,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Mswada huu unampa Rais mamlaka ya kuwateua watu wa kusimamia maswala yetu ya mahakama. Wenzangu waheshimiwa Wabunge watakubaliana nami shida si kwa sababu walioteuliwa walitoka jamii ya Wakikuyu au Wakamba. Shida ni kuwa hakuna mtu mmoja aliyeteuliwa kutoka kwa jamii fulani. Hiyo ndiyo shida kubwa ya uteuzi huu. Shida yetu ni kuzingatia ukabila katika uteuzi tunaoufanya katika nchi hii. Kuna baadhi ya watu wanaongozwa na hisia za kikabila katika maisha yao. Ningependa kuona Wakenya wakifanya kazi bila kuulizwa kwa nini katika idara fulani tuna Wakikuyu, Wakamba, Wajaluo, Waluhya au Waarabu wengi kuliko watu wa kutoka jamii fulani na kadhalika. Mambo haya yameleta hisia za ukabila. Ni Lazima kila Waziri awatumikie Wakenya bila kujali wanakotoka katika nchi hii. Kilicho muhimu ni kufuata sheria za nchi tunapotoa huduma kwa wananchi wetu. Kwa hivyo, ikiwa Jaji Mkuu atakuwa ameteuliwa kutoka jamii ya Waluhya, basi sisi sote tumuunge mkono na kufanya kazi naye. Nina hakika kuwa jaji huyo atafanyia Kenya kazi na wala hatawapendelea watu kutoka jamii yake. Ukabila hautajenga nchi hii. Hii ndio sababu ukabila sasa unazidi na unaenda mbele. Tukimteua mtu kufanya kazi katika Wizara ya Fedha, utaona yeye anataka watu wa jamii yake wafanye kazi naye. Hii ni kwa sababu anajua ya kwamba asipofanya hivyo, watu wake watamuuliza kwa nini hakuwasaidia alipokuwa katika wizara hiyo. Jambo kama hili huchangia ufisadi miongoni wa maofisa wa Serikali. Mambo haya tunayoyazungumza hapa ni mazuri sana, lakini hayatakuwa na maana kwetu ikiwa tutaongozwa na kasumba ya ukabila. Taifa hili litasaidiwa na watu wenye hekima wala si watu wa kutoka makabila fulani. Ni lazima ieleweke kuwa viongozi wetu wametoka katika jamii mbalimbali. Kwa mfano, tuna Rais kutoka jamii ya Wakikuyu, Waziri Mkuu kutoka jamii ya Wajalluo na Makama wa Rais kutoka jamii ya Wakamba. Huu ni ukweli wa mambo, lakini wao wana hekima ya kuiongoza nchi hii. Viongozi hawa wanatumikie nchi bila mapendeleo yoyote. Je, kwa nini orodha ya majina yaliyotajwa hapa haikuwa na mtu mmoja kutoka wale watu? Ndugu zangu, tuache udanganyifu na tuzungumze ili Wakenya wajue tunachosema. Usawa wa Wakenya ni kuwaakilisha Wakenya. Lakini kuleta mtu kutoka Somalia ili aje hapa kutusaidia ni uongo mtupu. Tutapigana na kuumizana. Tuzingatie mambo hayo. Mheshimiwa Waziri, ningependa kukueleza wazi kwamba ukitaka heshima yako, toa mambo ya wageni katika kitabu hiki. Iwapo wewe ni wakili katika nchi yetu ya Kenya na una heshima, utafanya nini kama Muafrika ikiwa huoni Mkenya anatosha? Mimi sijaona mambo kama hayo."
}