GET /api/v0.1/hansard/entries/166471/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 166471,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/166471/?format=api",
"text_counter": 262,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bwana Naibu Spika wa Muda, ningependa kumwambia Waziri--- Kwa kusema hivyo, nimepitia kwa Naibu Spika wa Muda. Nitarudia. Ningependa kumwambia Waziri kwamba mambo aliyoyaweka katika Mswada huu hayazingatii heshima ya Muafrika. Hatutaenda mbali. Nasema hivyo kwa nini? Mawakili wetu ni Waafrika. Kwa nini tuwe na mtu ambaye atazungumza na kukaa katika bodi hiyo ambaye atatolewa Somalia ama Zambia? Katika mataifa yote ya ulimwengu, Kenya iko katika orodha ya ramani ya dunia. Kenya inajulikana katika ramani ya dunia kwa sababu moja. Wafanyikazi nambari moja wako katika nchi hii. Wasomi wazuri katika bara letu la Afrika wako katika nchi hii. Hatuwezi kulinganishwa na watu wengine hata mkifanya nini. Leo hii, taifa hili lina upungufu wa wafanyikazi wenye ujuzi kwa sababu wanaajiriwa na kupelekwa nje wanapopewa mishahara mikubwa. Unapolinganisha wafanyikazi walio hapa na wale walioajiriwa nje, utaona kwamba wana tofauti kubwa. Sisi tuko mbele ya wengine. Ningependa kuunga mkono Mswada huu kwa kusema mambo hayo yaangaliwe na tupewe heshima yetu kama Waafrika na tuungane, tuzingatie umoja wetu. Ahsante, Bwana Naibu Spika wa Muda"
}