GET /api/v0.1/hansard/entries/166474/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 166474,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/166474/?format=api",
    "text_counter": 265,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Onyonka",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Foreign Affairs",
    "speaker": {
        "id": 128,
        "legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
        "slug": "richard-onyonka"
    },
    "content": " Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kweli, ni furaha yangu kuchangia Mswada huu. Mswada huu, kwa Wakenya wengi, ni wenye ghadhabu nyingi. Wananchi ambao tunawakilisha wamekuwa wakituuliza ni nini ambacho kinakera nchi yetu wakati huu ambao Rais Kibaki na Waziri Mkuu, Raila Odinga, wamechagua watu ambao wanatakiwa kutufanyia kazi, lakini inaonekana kuwa kuna shida. Kama mhe. Muthama amesema, shida ya Kenya ni kuwa na mafikira machanga ambayo si makubwa kuliko utu wetu binafsi. Kenya ni kubwa na inafaa sisi viongozi tuangalie shida ambazo zinatukabili ili tujaribu kuzitatua. Ukiangalia, utaona kuwa uteuzi wa mahakimu katika nchi hii ni shida kubwa. Kama viongozi, tupende tusipende, shida yetu ni kama ile iko kati ya wazungu na Afrika. Shida yetu ni ukabila. Shida zetu zimetokana na kuwa kila tukiwa na uongozi mmbaya, tunarudi kwa makabila zetu ili kuendeleza yale maovu ambayo tunafanya. Ninasema hivi kwa sababu mimi kama kiongozi kutoka Kitutu Chache, ningependa wananchi wajue hakimu mkuu ambaye wanamchagua anazungumza namna gani. Fikira zake ni zipi na makadirio yake ni yapi. Ningependa kujua fikira za yule ambaye atakayesimamia afisi ya mkuu wa mashtaka. Kwa kweli, Wakenya wengi wamejawa na ghadhabu kubwa na wanasikia vibaya kuwa Wakenya. Kesi ya fukara ikipelekwa kortini, hawezi kupata haki kwa sababu mahakimu wengine hawazingatii sheria. Kama wanavyosema, ukiwa na hela hapa Kenya, utainunua sheria na ukiwa maskini, utafungwa. Wakati huu, sheria imefika kiwango ya kuwa ukifanya makosa, unaweza kuzungumza na hakimu na mkakubaliane usikufungwe. Ni lazima tuangalie sheria ya Kenya na tuhakikishe kuwa mahakimu ambao watapewa kazi watachunga maslahi ya mwananchi wa kawaida. Hii itamfanya mwananchi wa kawaida awe na utu na akubali kuwa Kenya ni nchi ambayo anaweza kujivunia. Nitasema kinaga ubaga kuwa katika nchi yetu, hakuna mambo mengi sana ambayo tunajivunia. Ufisadi umejaa. Ni lazima tuwe na mahakama za haki na askari ambao watafuata sheria za nchi. Mwananchi akipelekwa kortini, angependa maslahi yake yalindwe, atendewe haki. Ingawa amevunja sheria, ni lazima apate haki yake, na yule ambaye amekosewa, apate haki yake pia. Ningependa kutoa shukrani zangu kwa Waziri Mutula Kilonzo. Yale mabadiliko ambayo Wabunge wameuliza kwa vifungu fulani, ningemuomba ayatilie maanani na kufanya marekebisho hayo. Ninasema hivi kwa sababu hatutaki tena kuwe na shida ama vuguvugu, tukiambiwa: “Rais aliseme hivi na Waziri Mkuu akasema hivi, lakini hao wawili bado hawajaelewana. Kwa hivyo hatujui ni watu gani wanaoteuliwa.” Tungependa ijulikane wazi ni akina nani wanaopendekezwa kwa vyeo hivyo ili kama ni uteuzi wa Jaji Mkuu, kwa mfano, tujue ili tuzungumzie mambo yake, baada ya Kamati ya Bunge kuujadili uteuzi huo na kukata shauri iwapo yeye ni mtu mzuri ama la. Tunataka tupewe majina hadharani, wananchi wakisikiza kwenye redio na kuona kwenye runinga zao; kwamba, mtu fulani alizungumza hivi na vile. Tukifanya hivyo, wananchi pia wataweza kuona kwamba sisi Wabunge tumechagua mtu mwenye hekima na heshima, na ambaye atayalinda masuala ya kikatiba yanayohusu sheria za nchi yetu ya Kenya. Bw. Naibu Spika wa Mda, nikimalizia, ningependa kuwatahadharisha Wabunge wenzangu wasije wakasahau kwamba chombo kinachotuelekeza kuyalinda maslahi ya nchi yetu ni Katiba tuliyoipitisha hivi majuzi; na kwamba iwapo Bunge hili halitakuwa lenye heshima na kuilinda Katiba, pamoja na maslahi ya Wakenya, historia itatuelekezea kidole chenye lawama. Ni lazima tuhakikishe kwamba tumeilinda heshima yetu, tukiwa Wabunge waheshimiwa, kwa kupitisha sheria zenye manufaa kwa Wakenya wa kawaida, na kuacha kuzingatia maslahi ya Wakenya matajiri pekee, walio wachache. Ahsanteni."
}