GET /api/v0.1/hansard/entries/167127/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 167127,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/167127/?format=api",
"text_counter": 604,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, naomba kutoa maoni yangu kuhusu Mswada huu. Jambo la kwanza, naomba tujiulize, kama Wakenya, ni nini tunataka? Tunataka maridhiano ama ni nini? Kama ni maridhiano, tutayapata vipi? Je, tumewauliza wananchi ni nini wanachopendelea, ama tumejitwika wajibu wa kuamua kwamba hili ndilo linalofaa katika nchi hii? Jambo la pili, mambo mangapi ambayo hivi sasa yamekita mizizi nchini humu, na hamna lolote mnalofanya? Mawaziri wenyewe pia hawana imani na mahakama yetu. Je, mtawaelezaji Wakenya kuwa mkianza mahakama hayo hapa nchini watu watakuwa na imani nayo? Nimesikia mengi yakizungumzwa. Jana Waziri alinena kwamba tukiunda mahakama hayo sisi wenyewe tutayabana hapa, na tutaweza kuyaendesha vile tutakavyotaka. Je, wananchi watakuwa na imani gani na hayo mahakama?"
}