GET /api/v0.1/hansard/entries/167128/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 167128,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/167128/?format=api",
"text_counter": 605,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Jambo la tatu, naomba tufikirie kidogo tu mambo ambayo yalitokea baada ya uchaguzi mkuu liopita. Baada ya watu kupigana na kuraruana ni nini kimefanyika? Kuna watu ambao wameshikwa? Kuna watu ambao mpaka sasa hawajahukumiwa? Kwani hakuna sheria ya kuwahukumu hao watu? Kama sheria ipo, mbona hawajahukumiwa? Mbona wamewachiliwa hivi hivi. Watu bado wana uchungu. Sasa mnasema kwamba tuwachane na hayo mambo, na tuanzishe mahakama ambayo yatakuwa na wageni na Wakenya. Je, hao wageni wakiwa hapa, hamwezi kuwatia mfukoni? Hii imekuwa ni tabia ya Wakenya; hata kukitokea kashfa gani, iwe ni ya mahindi ama mafuta, watu wanaachiliwa kwenda zao. Je, nauliza, imani ya watu wa Kenya itaregeshwa namna gani? Hamwezi kuirekebisha. Ni lazima hao watu waende Hague. Wacha waende wahukumiwe huko. Kama tumepatikana na makosa, tunaogopa nini? Kama unajihisi kwamba haujahusika na lolote baya, wasiwasi wako ni wa nini? Kama unajua huna lolote ambalo umemkosea mtu, shida yako ni nini?"
}