GET /api/v0.1/hansard/entries/167129/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 167129,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/167129/?format=api",
    "text_counter": 606,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, kama Wakenya tukubali kwamba kuna mambo mengi ambayo yametendeka. Tukiangalia Mkoa wa Pwani, watu hawana haki ya mashamba yao. Watu wetu wa Pwani wanapendelea kwamba hao watu wapelekwe huko huko kujibu mashtaka yao. Hapa nchini hakuna haki. Haki iliisha. Tumekutana hapa na tukajadiliana mambo mengi ambayo yanaweza kujenga nchi na kuleta maridhiano. Lakini ni hatua gani ambayo Serikali imechukua kufanya watu waridhiane? Juzi tumepitisha sheria kuhusu haki, ukweli maridhiano na tume . Hivyo inamaanisha kwamba hata watu wakiridhiana, bado kuna kipengele kinachosema kwamba kama mtu hataki kumsamehe mwenzake, huyo mwenzake atapelekwa mahakamani. Mbona hatukufuata mfano wa Afrika Kusini, kwamba watu waridhiane tu. Sisi tuna sheria inayowataka kuridhiana, lakini kama mtu hajaridhika basi sheria inamkubalia kwenda mahakamani."
}