GET /api/v0.1/hansard/entries/167134/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 167134,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/167134/?format=api",
"text_counter": 611,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Katika mwaka 1992, baada ya uchaguzi mkuu, Wakenya waliuawa. Baadaye kuliundwa kamati ambayo ilikuwa chini ya uwenyekiti wa Bw. Kiliku. Mpaka leo hakuna ambaye anajua kilichoandikwa na kiko wapi. Mwaka 1997, vile vile Wakenya walipiga kura ili kuwachagua Wabunge na Rais. Mwishowe, baada ya Wakenya kuuawa, tume ya Jaji Akiwumi iliundwa. Hakuna chochote kilichofanyika. Ripoti ya tume hiyo iliwekwa na bado \"inalala\". Mwaka 2002, baada ya uchaguzi, Wakenya waliuawa. Hakuna mtu hata mmoja aliyepelekwa mahakamani. Juzi, katika 2007, kiwango cha mauaji kilizidi kutoka asilimia kumi hadi themanini, na hakuna mtu mpaka leo amepelekwa mahali popote. Ni dhahiri kwamba sisi kama taifa tumeshindwa na tumekoma kabisa kujifanyia mambo yetu. Kwa hivyo, ilibidi tuite wageni kutoka nje ilihali tuna wasomi wa Sheria. Tuliwaita wageni kutoka nje Fe bruary 5, 2009 PARLIAMENTARY DEBATES"
}