GET /api/v0.1/hansard/entries/167137/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 167137,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/167137/?format=api",
"text_counter": 614,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, tumeona na ni dhahiri kwamba katika koti zetu--- Kuna wakati mmoja watu walipelekwa kortini, sitasema majina yao, na wakafanya njama ya kuleta watu wao kutoka nyumbani wakajaa katika korti mpaka Jaji akashindwa kufikia mlango wa kupitia. Hivi leo, ni dhahiri kwamba uamuzi wa Wakenya, mahali popote walipo, hawataki kusumbuliwa na kusikia kwamba Jaji atakayeshughulikia kesi za uuaji ni Mkamba ama Mkikuyu, kwa sababu tumeshindwa kung'oa, kukanyaga na kuchoma mizizi ya ukabila katika nchi hii. Ni vyema tugeuze mbinu zetu kidogo ili kuwaonyesha wale ambao huuwa wengine kwamba ndege zitakuja, watawekwa ndani na kupelekwa kule, na kuiacha nchi hii ikiwa na amani."
}