GET /api/v0.1/hansard/entries/16855/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 16855,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/16855/?format=api",
    "text_counter": 300,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mung’aro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 76,
        "legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
        "slug": "gideon-maitha"
    },
    "content": "Jambo la ya nidhamu, Bw. Spika. Swali la pili katika ratiba itakayofuata ni uteuzi wa Baraza la Mawaziri. Kama tunavyojua, Serikali yetu ni ya Mseto na kila mrengo wa Serikali hii ya Mseto huwateua Mawaziri wake. Ningetaka kupata mwongozo kutoka kwako: Tunajua kwamba, Waziri Mkuu anahusika na usimamizi wa Baraza lote la Mawaziri lakini hahusiki na uteuzi wote wa Baraza la Mawaziri. Je, atajibu maswali kuhusu suala hili kama msimamizi wa Baraza la Mawaziri ama kama mteuzi wa Baraza la Mawaziri ama katika mrengo wake wa Baraza la Mawaziri?"
}