GET /api/v0.1/hansard/entries/169927/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 169927,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/169927/?format=api",
"text_counter": 434,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "jambo hilo litakuwa la maana sana. Ningetaka kumshukuru na kumtambua aliyekuwa Waziri wa Serikali za Wilaya, Marehemu Karisa Maitha, kwa maana alipokuwa Waziri alileta Mswada hapa wa kupendekeza madiwani walipwe na Serikali kuu. Wakati huo, alipendekeza walipwe Kshs250,000 kwa mwezi. Labda pesa hizo haziwezi kupatikana leo lakini kuna umuhimu wa kujadili swala hili. Madiwani katika nchi ya Kenya ni 4,000 na hata kama wanaweza kulipwa Kshs150,000, kwa ujumla, pesa hizo haziwezi kupita Kshs4 milioni. Hizo ni pesa ambazo Serikali, kama kweli inaweza kuimarisha utawala katika maeneo ya udiwani katika nchi hii, inaweza kulipa. Imeonyesha kwamba inaweza kulipa mishahara mikubwa kwa watu fulani. Madiwani wengi wamesoma. Wanasimamia shughuli zote mashinani. Kwa hivyo, ningetaka madiwani wetu walipwe mishahara mizuri. Ninependekeza walipwe Kshs150,000."
}