GET /api/v0.1/hansard/entries/173337/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 173337,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/173337/?format=api",
"text_counter": 380,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Kwanza, ninamwomba Waziri aangalie kampuni za meli ambazo zimeandikishwa humu nchini kwa maana nyingi zao zinasafirisha mizigo. Ninamwomba Waziri aangalie kampuni za meli katika nchi jirani ya Tanzania. Hamna kampuni ya meli inayoruhusiwa kuwa na kampuni nyingine ndogo ndogo za kusafirisha mizigo bila kuwahusisha wenyeji. Ukiangalia katika nchi yetu ya Kenya, utaona kwamba kampuni nyingi za meli zinasafirisha mizigo ndani na nje ya nchi. Je, wananchi wameachwa wapi? Hamna lolote wananchi wanafaidika kutoka kwa kampuni hizi ambazo zinasafirisha mizigo ndani ya nchi."
}