GET /api/v0.1/hansard/entries/173543/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 173543,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/173543/?format=api",
"text_counter": 586,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Haji",
"speaker_title": "The Minister of State for Defence",
"speaker": {
"id": 26,
"legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
"slug": "yusuf-haji"
},
"content": "Tunasoma kwa gazeti na kuona kwa televisheni vile watu wengi wanateseka kwa sababu ya njaa. Wakati mwingine unaona kuwa ni dhambi kubwa sana kula chakula. Ni lazima walimu watafakari sana kwa sababu haina faida yoyote kwao na kwa nchi pia kudhalilisha watoto ambao hawana dhambi na wanataka kusoma. Wanaweza kuendelea kufunza na pia watafute haki yao vile inavyopaswa. Adhuhuri ya leo, Kaimu Waziri wa Fedha aliomba Bunge hili lipatie Serikali hii ruhusa ya kukopa Kshs7 bilioni. Makosa mawili hayafanyi moja kuwa sawa. Makosa ni makosa. Kama kweli kuna tuhuma ya kwamba mahindi yanatumiwa kwa njia mbaya, yameibwa na hii ni fikira ya watu wengi sana, ninajua ya kwamba Serikali inafanya uchunguzi. Tunatarajia ya kwamba wale ambao wanahusika watatajwa hapa na hatua kali itachukuliwa. Hakuna msamaha ambao utatolewa kama vile mara nyingine ambapo watu wanafanya makosa kama hayo na wanapewa msamaha."
}