GET /api/v0.1/hansard/entries/174276/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 174276,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/174276/?format=api",
"text_counter": 588,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mungatana",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Medical Services",
"speaker": {
"id": 185,
"legal_name": "Danson Buya Mungatana",
"slug": "danson-mungatana"
},
"content": "Jambo la tatu ambalo tunaweza kujifunza ni kwamba tunaweza kuchagua kiongozi wa nchi, ambaye hajahusika na mambo ya ufisadi. Barack Obama amechaguliwa kuwa kiongozi wa Marekani na hajatajwa katika kashfa za ufisadi. Kwa sasa ni lazima tujifunze kwamba kuna watu ambao tunatarajia kwamba watataka urais, na sasa wanaingizwa katika maneno ambayo hayafai. Katika Kenya hii tumesikia kwamba kuna watu wanaokula mahindi ya maskini. Ni aibu kwamba wakati huu ambapo dunia nzima inaangalia Wakenya, kuna vichwa vya magazeti vinavyosema kwamba kuna ufisadi nchini Kenya. Kuna wengine ambao wanataka ukubwa ilhali wanahusika na kashfa ya mafuta. Tumesikia kashfa ya mahindi hapa Kenya ni zaidi ya billioni moja."
}