GET /api/v0.1/hansard/entries/174364/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 174364,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/174364/?format=api",
"text_counter": 676,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Nataka kusema kwa kifupi kwamba kuchaguliwa kwake Bw. Obama kulitokana na matamshi yake ya kweli, kusikia sauti ya Wamerikani na kuwaambia pahali wanapoelekea na kule anakotaka kuwapeleka. Nataka kuwaomba viongozi wote, hasa wanaotaka uongozi wa nchi hii, tafadhali wajifunze; katika kampeni zitakazokuja, Mungu akitujaalia, tuwe na viongozi ambao wanaweza kutuahidi mambo watakayoweza kuitendea nchi hii. Hatutaki kuombwa kura na watu kwa sababu wamejaribu mara nyingi, wamekuwa pale, ni wazee au wanataka kulipwa kwa kazi waliofanya. Naomba tuwe na viongozi watakao omba kura kwa sababu watakuwa na maono kama kutuambia kuwa kwamba wakiwa rais watatupa elimu, na waahidi kwamba wasipofanya hivyo katika miaka miwili watajiondoa uongozini. Si mambo ya kusumbuka! Tumesumbuka kwa zaidi ya miaka 45 na maji yako kule kule. Hii ni kwa sababu tunapiga kura bila kujua mambo tunayoweza kumwambia kiongozi tunayemtaka. Bw. Obama aliwaambia Wamerikani kuwa atawapatia mabadiliko na ndio sababu walimpigia kura."
}