GET /api/v0.1/hansard/entries/174519/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 174519,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/174519/?format=api",
"text_counter": 42,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Machage",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Roads",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": " Mhe. Spika, ninaunga Hoja hii na ni ruhusu niseme yafuatayo. Mhe. Spika, kitendo ambacho kimetendwa leo ni cha hekima. Wale walioteuliwa wasijivune bali wajue wao ni watumishi wa Bunge hili. Watutumikie kwa uzuri, wema na hekima. Hii ni kwa sababu kila mmoja hapa alikuwa na uwezo huo wa kutumikia wananchi wa Kenya na Bunge hili kama wangeteuliwa. Mhe. Spika, tukumbuke ya kwamba jana tulipitisha Mswada ambao umestaafisha wale waliokuwa wakifanya kazi katika Tume ya Uchaguzi. Bunge hili halikutoa amri ya kuwasulubisha wala wengi wao hawakufanya makosa. Wafanyakazi wengi ambao wataenda nyumbani ni vijana ambao waliteuliwa miezi michache sana kabla ya uchaguzi wa Kenya kufanywa. Hawana hatia kwa Wanakenya. Ombi langu kwa wale ambao wamepewa jukumu la kuangalia masilahi ya wafanyikazi wa Serikali ni kwamba kila mtu apewe haki yake akistaafishwa. Sisi katika Bunge hatukusema kwamba wasije wakapewa marupurupu yao. Hatukusema hivyo! Kwa hivyo, mtu huko nje asije akasema kwamba Bunge lilisema kwamba wale makamishina waliostaafishwa hawatapata haki yao. Huo utakuwa uzembe, ubaradhuli na 4182 PARLIAMENTARY DEBATES December 17, 2008 kunyanyasa wengine. Mhe. Spika, tunataka Kamati ambayo imeteuliwa siku ya leo iwe na utu. Isije ikajitapa kwamba ina uwezo zaidi. Tunataka kuona uzuri wao tu. Ni lazima watambue kwamba katika nchi hii, kuna jamii ndogo, jamii za watu wachache, jamii ambazo zimenyanyaswa na kusahaulika katika nchi hii kwa muda mrefu. Historia itadhibitisha mambo hayo. Kwa hivyo, wanapoteua kamati ambazo wamepewa wadhifa wa kuteua, wajue kwamba Wakenya wanawaangalia kwa uadilifu kabisa. Wasije wakaonekana wabaya. Hii ni kwa sababu hata kama watajificha, ni heri waelewe kuwa kizuri kitajiuza na kibaya kitajitembeza tu. Ninasema jambo hilo pia kwa wenzetu humu Bungeni. Wakati mwingi tumepata shida na waandishi wa habari kwa sababu wenzetu wengine hapa wanajifanya watakatifu na wazuri zaidi ya wengine. Wanajitapa kila wanapopata nafasi na kujisifu na kujitukuza."
}