GET /api/v0.1/hansard/entries/174549/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 174549,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/174549/?format=api",
"text_counter": 72,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister of State for Special Programmes",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Ahsante sana, mhe. Naibu wa Spika kwa kunipa nafasi hii kuzungumza juu ya Hoja hii. Ni muhimu kwetu kwenda nyumbani na kujiunga na wenzetu kusherehekea sikukuu ya Krismas na watu waliotuchagua kuja hapa Bungeni. Huu ulikuwa mwaka wa matatizo. Hata hivyo, ningependa kuwaambia waheshimiwa Wabunge wenzangu kwamba matatizo hayo yawe ni funzo kwetu, ili tuweze kuwaunganisha wananchi wetu. Wiki mbili zilizopita zimenifunza mambo mengi sana. Tumeweza kukaa pamoja kama waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Kumi na kuzungumza kama Wakenya na wala si kuzungumza kama watu wa makabila mbali mbali. Kwa hivyo, ningependa kuwapongeza Wabunge wote kwa shughuli hii tuliyoifanya na kuanzisha msafara wa kuiwezesha nchi hii kupata Katiba mpya. 4190 PARLIAMENTARY DEBATES December 17, 2008 Bw. Naibu wa Spika, jambo ambalo ningependa kusema siku hii ya leo, tukielekea kwenye shughuli za sikukuu ya mwisho wa mwaka, ni kwamba masikilizano yetu yalianzishwa na mhe. Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu, mhe. Raila Odinga na waakilishi wetu wa Mkahawa wa Serena. Ni kutokana na mkataba wao ndio tumefika pahala tulipo sasa hivi. Ningependa kuwauliza waheshimiwa Wabunge wenzangu kwamba tunapoelekea nyumbani tujaribu sana kuwaunganisha Wakenya. Kamati ya Bunge tuliyoichagua hapa itakuwa ikikaa kuzungumzia maswala ya barabara tutakayofuata ili tutengeneze Katiba kielelezo. Ni muhimu sisi kama waheshimiwa Wabunge kuendelea kuiunga mkono Kamati hii, ili waweze kutengeneza Katiba kielelezo itakayokubaliwa na wananchi wote kwa kauli moja. Hapa Bungeni tumepitisha sheria nyingi zinazohusu maisha ya Wakenya wote kwa jumla. Bw. Naibu wa Spika, Katiba ya Kenya ni muhimu sana. Katiba ndiyo inayotupa msingi maalum kama Wakenya. Kwa hiyo, Katiba yetu ni msingi wa nchi hii. Kwa hivyo, tuungane ili tuweze kutengeneza Katiba ambayo itaunganisha nchi yetu. Tujaribu sana tusirudie ule mchezo uliokuwepo kule Bomas of Kenya. Ninamtakia kila mtu kila la heri tunapokwenda nyumbani. Ninaomba kwamba tuendelee kuwazungumzia wananchi huko nyumbani, yale yote tuliyojifunza katika wiki hizi mbili. Tukizungumza juu ya maendeleo, pia tuzungumze juu ya umoja wa Wabunge wa Bunge hili la Kumi. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}