GET /api/v0.1/hansard/entries/174561/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 174561,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/174561/?format=api",
    "text_counter": 84,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ms. S. Abdallah",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 380,
        "legal_name": "Shakila Abdalla",
        "slug": "shakila-abdalla"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja ya leo ambayo inatupatia nafasi ya kuenda nyumbani kwa mapumziko kidogo. Jambo la kwanza, ninataka kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufika hapa leo tukiwa kwenye Jumba hili la kifahari. Bw, Naibu Spika, kitu cha pili ni kuwapongeza wale ambao wamechaguliwa kwa ile kamati ya leo kusimamia maswala ya mambo ya tume ya uchaguzi na Katiba mpya. Ningependa kuwakariria wale ambao tumewapatia hayo majukumu kwamba, tumewapatia majukumu kwa imani kama Wabunge na tumefanya uamuzi huo kwa wajibu wa wananchi wote wa Kenya. Ni wajibu wao watekeleze majukumu yao kwa njia ya haki wakizingatia haki zote za nchi. Wajue kwamba Kenya ina makabila mengi na wazingatie hayo yote. Pia tunajua kati ya wale ambao tumewachagua ni changamoto kwao. Tunajua kuna wengi ambao wana matarajio yao ya kibinafsi lakini tumewachagua kwa imani. Tunataka waangalie nchi na waache kufikiria matarajio yao ya kibinafsi na wawe pale kwa niaba ya nchi na wananchi, ili Bunge la Kumi lilete mabadiliko ya uongozi kwa nchi hii yetu ya Kenya ambayo wananchi wengi December 17, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 4195 wanatarajia. Bw. Naibu Spika, jambo lingine ni kwamba waangalie pia maswala ya mazingira na mambo mengi muhimu, ambayo yataunganisha nchi kufanya kitu kimoja. Ninataka nitoe shukrani pia kwa Serikali kwa kuamua kutujengea bandari huko Lamu. Ningechukua nafasi hii kusema kwamba hiyo bandari iwe ni jambo ambalo litatufaidi sisi watu wa Lamu, kwa sababu watu wengi wameadhirika na madawa ya kulevya na majanga ya njaa. Kwa hivyo, ni matarajio yetu kwamba hiyo bandari itatutoa kwenye majanga ya njaa na utumiaji wa madawa ya kulevya, kwa sababu hilo ndilo jambo ambalo limeadhiri sana vijana wetu huko Lamu. Jambo lingine muhimu ambalo ningependa kuongezea ni swala la chakula. Chakula ndio shida kubwa. Ningependa kusema kwamba ule unga ambao umesemekana kwamba ni wa bei ya chini uwafikie watu mashinani, kwa sababu hao ndio wenye shida zaidi kuliko watu wa mijini. Tusiangalie unga pekee yake; tunajua kwamba Wakenya wanatumia vyakula vingi na ni muhimu Serikali iweke taratibu za bei ya chakula, ili Wakenya waweze kufikia chakula kwa njia ya urahisi na kulingana na mapato yao. Kuna wengi wanatumia chakula kama mchele, viazi na kadhalika. Kwa hivyo, tusiangalie unga peke yake, ijapokuwa unga ndio chakula ambacho ni rahisi kwa sasa, lakini bei yake sasa imepita ya mchele. Kwa hivyo, tunaomba Serikali iweke mikakati ya kusimamia bei ya chakula. Hili ni jambo litakalowafaidi wananchi. Bw. Naibu Spika, jambo lingine ni kwamba tuwe tukiangalia jambo la kuinua makabila bila kuangalia kama ni madogo au makubwa. Tuungane kama Wakenya na tuweke kando ukabila na tuangalie zile shida zinazotukabili, ili tuweze kuzitatua kwa njia mwafaka bila kufikiria hili kabila ama lile linafaa, liko hivi ama vile. Kwa hayo machache, ninawatakia nyote Krismasi njema na mwaka mpya wenye mafanikio."
}