GET /api/v0.1/hansard/entries/174582/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 174582,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/174582/?format=api",
"text_counter": 105,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Yakub",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 378,
"legal_name": "Sheikh Yakub Muhammad Dor",
"slug": "sheikh-dor"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii ili nichangie Hoja hii. Ningependa kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia sote kufika Mwezi huu wa Desemba kwa afya njema. Pia ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru Bw. Spika na wewe Bw. Naibu Spika kwa kazi njema mliotufanyia mpaka sasa. Jambo muhimu ambalo tungetaka Wakenya watambue ni kwamba, baada ya Mswada wa kurekebisha Katiba wa mwaka 2008, kwa mpangilio uliopitishwa na kuona kwamba tulikuwa na vikao vya Wabunge vya Kamukunji kwa siku, imeonyesha dalili ya kwamba kuna Wambunge katika Bunge la Kumi ambao wameamua kwenda kwa mpangilio wa kuangalia haki na sio kwa mipangilio kama Bunge za hapo awali. Bw. Naibu wa Spika, kuhusu Mswada huu ambao ulipita, ningependa kuchukua nafasi hii kuwafahamisha waheshimiwa Wabunge wenzangu na ile Kamati iliyochaguliwa kwamba wale wafanyikazi wa Tume ya Uchaguzi 600 ni Wakenya. Wengi wao hawakuwa na makosa yoyote yaliyosababisha kuingia kwao kwenye wimbi la kufutwa kazi. Kwa hivyo, twataraji kwamba watafikiriwa kwa njia za haki, kukizingatiwa kwamba wao pia ni Wakenya walio na familia. Itakuwa ni shida kwao kuangalia familia zao kwenye maswala ya elimu na afya zao, na maswala mengine ya nyumba zao bila kazi. Kwa hivyo, ningependa kuwepo na mpangilio mwafaka. Tusiwe na mpangilio wa mazungumza tu. Baadhi yao wanaweze kuajiriwa na Serikali au tume mpya ya uchaguzi itakayoundwa. Wale ambao hawatapata nafasi ya Serikalini, wapewe marupurupu yao kuambatana na sheria zetu. Jambo lingine ambalo ningependa kulichangia ni kifungu kinachosema kutakuwa na tume ya kuangalia maeneo ya uwakilishi Bungeni. Ninawaunga mkono Wabunge wenzangu waliokuja na fikira ya kwamba tusiangalie idadi ya watu peke yake. Kuna umuhimu sana wa kuangalia ukubwa wa maeneo pia. Kuna maeneo ambayo ni makubwa mno, lakini watu ni wachache. Hiyo haimaanishi kwamba mhe. Mbunge kutoka eneo kama hilo kazi zake zimekuwa chache. Mbunge kutoka eneo kubwa lenye watu wachache huwa ana kazi nyingi zaidi kuliko Mbunge ambaye ana eneo ndogo lenye watu wengi. Nataraji kwamba fikira hiyo itazingatiwa. Idadi ya ziada wa Wabunge wapya itaenda kwa mfumo wa kila mkoa kupewa nafasi kulingana na ukubwa wa maeneo yao. Bw. Naibu wa Spika, ninaishukuru Serikali kwa mipango ya maendeleo ya mwaka ujao. Mmoja wapo ukiwa mpango wa kujengwa kwa bandari mpya kule Lamu. Hilo ni jambo zuri sana. Wale ambao ni wajuzi katika maswala ya bandari wamesima kwamba bandari itakayojengwa 4204 PARLIAMENTARY DEBATES December 17, 2008 Lamu itakuwa kubwa zaidi, na yenye uwezo wa kupokea meli kubwa kuliko meli ambazo zinaingia kwenye Bandari ya Mombasa. Hata hivyo, ningependa kuileza Serikali kwamba watu wa Lamu hawajaweza kuisherehekea fikira hiyo. Sababu kubwa ni kwamba wakazi katika sehemu hiyo mpaka sasa hawana vyeti vya umiliki wa ardhi. Watu ambao si wakazi wa Lamu wanafurahia mpango huo wa kujengwa kwa bandari mpya. Hata hivyo, wenyeji wa Lamu hawajafurahia fikira hiyo ingawaje hiyo ni fikira itakayoleta maendeleo makubwa katika Lamu na nchi yote kwa jumla. Itapunguza ukosefu wa ajira na kuondosha umaskini katika Wilaya ya Lamu. Wenyeji wa Lamu hawajaona kwamba maendeleo hayo yakifanyika yatawafaa wao watu wa Lamu. Kwa hivyo, tunaiomba Wizara ya Ardhi iwafikirie kwa haraka wakazi wa Lamu kuhusu suala la haki ya umiliki wa ardhi. Kwa hayo machache, ninaunga Mkono Hoja hii."
}