GET /api/v0.1/hansard/entries/174588/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 174588,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/174588/?format=api",
    "text_counter": 111,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika. Nasimama kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa wakati alionipa kuona mwaka huu ukiisha, kuwa hapa Bungeni na kuwa na marafiki wengi na kuweza kuchangia Hoja nyingi, na kwamba yote haya yameenda sambamba. Bw. Naibu Spika, nataka kuzungumzia masaibu ya wananchi tukifunga mwaka. Nataka kusema kwamba hivi sasa tukifunga mwaka kuna wananchi waliofurushwa kutoka makwao na bado wanakaa viwanjani. Wanazalia viwanjani na kuumwa na mbu, ilhali sisi tuko hapa. Tunapofunga mwaka na kusema tunaenda likizo, tunawaacha watu wale wakiteseka. Sisi tunaenda Krismasi na hata tunatuma salamu, lakini tunasahau kwamba kuna wananchi ambao ni wakimbizi wa kisiasa katika nchi yao. Nataka kusema kwa kweli kwamba hata tunapoenda Krismasi, hakuna usawa kamwe. Hakuna jambo hata moja tunaweza kusema tunajivunia kama watu zaidi ya 30,000 bado wanateseka baada ya kupata uhuru miaka 45 iliyopita. Bw. Naibu Spika, nataka kuzungumzia masaibu ya chakula. Tunapozungumza, hivi sasa, wale wananchi ambao tulipigania sana hapa, ili bei ya chakula ipungue, bei bado ingali iko juu. Ukienda sokoni hakuna chakula. Tunazidi kusema kwamba kuna chakula, ilhali kwa maduka hakuna. Wananchi bado wanateseka huku tukienda likizoni. Ni juu yetu kuhakikisha kwamba shida hii imetatuliwa. Jambo la tatu ni kwamba wananchi wanaudhika na Wabunge wao na Serikali. Wananchi wanalalamika juu ya masaibu yao. Wakipita hapa na wakiona magari ya kifahari tulioweka hapa nje yakiwa yamejaa uwanja huu, wanaona kwamba hawa ni wale watu wanaokula pesa tulizowapa. Nataka kusema kwamba, jambo lilofanyika mwakani lilikuwa nzuri kwa sababu nchi ilikuwa katika mutaharuko na msukosuko mkubwa wa taabu. Lakini mbali na hayo, tuliweza kusukuma December 17, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 4209 Serikali yetu na kuunda Serikali ya Mawaziri 40. Ni aibu kwamba, hivi sasa, kuna magari ya kifahari 40 katika kila Wizara na mengine ya kuwafuata nyuma, huku wananchi wetu wakiwa bado wanateseka kule nje. Hili jambo linataka lifikiriwe. Kama nchi hii ni masikini na haijitoshelezi, inafaa wote tuishi kama watu ambao tunajua tunakoenda. Bw. Naibu Spika, jambo la nne ni kwamba tunahitaji tutambue ni watu gani tunaongoza kwa uwezo wao, au nguvu zao ni zipi. Tunatakikana hata kuzungumzia mambo ya katiba na kuwaeleza juu ya sheria. Mambo ambayo tunazungumzia kwamba tutaleta katiba mpya ni kizingizio tu cha kutafutia watu kazi kwa kuunda tume kadhaa na mwananchi bado anateseka. Bw. Naibu Spika, nataka kuzungumzia mambo ya kodi. Hivi sasa Wabunge wanaonekana kama ni watu ambao ni wahuni na hawasikii sauti ya wananchi. Kulipa kodi ni kawaida, na tumeeleza kwamba kifungu ambacho kinasema uwe mwaminifu kwa nchi yako kiko, na kinakulekeza kwenda kulipa kodi. Kipengele kilichowekwa Bungeni kinasema kwamba mtoza ushuru asimfuate mtu kama si mwaminifu kwa nchi yake. Mpaka wakati ambapo tutaanza kulipa kodi, hatuna sura katika nchi yetu. Mimi nimeanza na nitaendelea kulipa na ninataka wenzangu walipe. Pesa hizi tutawacha hapa duniani, hata uwe na ngapi. Pale utakapoenda katika chumba chako cha kuzikwa, utakuwa mfuko mtupu, na hata senti moja ikilia ukipelekwa kaburini itatolewa na kuwekwa kando. Pesa hizi ni za kusaidiana. Inatoka mkono huu, inaingia mkono mwingine, na tusipendelee zaidi. Jambo la mwisho ni kwamba waalimu wetu wana shida na hivi sasa wanatishia kwamba watagoma kwa sababu wanataka mshahara uongezewe; kwa hivyo wanalia. Kwa wazazi nao karo imeongezwa shuleni. Nataka kutoa mwito kwa Bunge hili kwamba tukirudi hapa, mambo yetu tuache kando na tuingilie mambo ya wananchi ili tukirudi nyumbani tuonekane kwamba sisi ni vyongozi na tunaongoza watu ambao tunawafahamu. Ningependa kusema kwamba ikiwa mtu ana familia yake, na mke wake ana vidonda vya tumbo na watoto wana maradhi ya kuendesha, na huku anaenda dukani kununua chakula ambacho kimewekwa pilipili, basi analisha jamii yake chakula ambacho hakiwafai. Ninatoa mwito kwa Wabunge wote kwamba tuwe waaminifu kwa nchi yetu."
}