GET /api/v0.1/hansard/entries/175383/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 175383,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/175383/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kiunjuri",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Water and Irrigation",
"speaker": {
"id": 175,
"legal_name": "Festus Mwangi Kiunjuri",
"slug": "mwangi-kiunjuri"
},
"content": " Bi. Naibu Spika wa Muda, naomba kujibu. (a) Wizara yangu, kupitia shirika la National Water Conservation and Pipeline Corporation (NWCPC), imekuwa ikichukua hatua za kurekebisha mabwawa yaliyozibwa na mchanga Wilayani Samburu. Kutoka mwaka 2005, mabwawa 12 yamerekebishwa, na katika mwaka huu wa Kiserikali mabwawa tisa yatarekebishwa. Pia kuna mpango wa kujenga mabwawa 12 kupitia shirika la Ewaso Nyiro North Development Authority. (b) Wizara yangu itachimba visima vitatu katika eneo la Samburu Mashariki na Samburu Magharibi mwaka huu wa Kiserikali. Visima vingine vinne vinaendelea kuchimbwa Wilayani Samburu Kazikazini. Kazi hii inafanywa kwa kutumia fedha kutoka shirika la Water Services Trust Fund."
}