GET /api/v0.1/hansard/entries/176936/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 176936,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/176936/?format=api",
"text_counter": 112,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Rai",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 203,
"legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
"slug": "samuel-rai"
},
"content": "Bw. Spika, ninakubaliana na mhe. Leshomo. Jambo hili lilifanyika wakati Bunge lilikuwa limevunjwa na hatukuwa na Mbunge katika sehemu hiyo. Wakati wa kuunda kamati hizi, ni lazima Mkuu wa Wilaya, Mbunge wa sehemu hiyo, Ofisa wa Kilimo, Karani wa Wodi, Ofisa wa Ardhi, Ofisa wa Mipango na madiwani wawe wanahusika katika mipango hii. Hata hivyo, wakati huo mambo haya yalipofanyika hakukuwa na baraza la madiwani au Mbunge. Ninamuomba mhe. Leshomo radhi. Mambo haya yamefikishwa katika Wizara na tayari tumetoa ilani ya urekebishaji. Ninaamini kwamba maofisa hawa wakikaa, wataleta orodha ya majina iliyo sahihi, ili tuyatangaze katika Gazeti rasmi."
}