GET /api/v0.1/hansard/entries/176937/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 176937,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/176937/?format=api",
    "text_counter": 113,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. K. Kilonzo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 172,
        "legal_name": "Julius Kiema Kilonzo",
        "slug": "kiema-kilonzo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Ningetaka kumshukuru Waziri Msaidizi kwa kujibu Swali hilo. Katika sehemu \"a\" ya Swali, mhe. Leshomo ameuliza: \"Je, ni mbinu gani hutumiwa--- ?\" Kuna shida kubwa wakati wa uteuzi wa wazee wanaohusika na mambo ya ardhi. Wakati mwingi, wanachaguliwa miongoni mwa watu ambao hawatakikani na wananchi. Je, Wizara inaweza kuangalia mbinu za kuwahusisha wananchi katika uchaguzi huu? Wakati fulani, tulikuwa tumelegeza sheria za kuchagua maofisa hawa. Bw. Spika, hivi sasa, tumesema kwamba ni lazima mwenye kuchaguliwa awe na miaka 3834 PARLIAMENTARY DEBATES December 3, 2008 zaidi ya 35, bila makosa yoyote ya uhalifu, mwenye cheti cha Kidato cha Nne na awe ameifanyia kazi Serikali."
}