GET /api/v0.1/hansard/entries/178551/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 178551,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/178551/?format=api",
"text_counter": 311,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Kutuny",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 61,
"legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
"slug": "joshua-kutuny"
},
"content": "Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Mimi kama mkulima mashuhuri nina masikitiko makubwa juu ya hali ilivyo katika nchi hii. Nimevuna zaidi ya magunia 1,000 ya mahindi. Sehemu yangu ya uwakilishi Bungeni ya Cherangany ina chakula kochokocho. Hata hivyo, malalamiko yetu ni kwamba Serikali haijaweka mikakati ya kuwezesha sisi wakulima kuuza mazao yetu kwa bei ya juu. Sisi huwatazama kwenye runinga watu wa Kibera wakilalamika kwamba bei ya chakula imeongezeka maradufu. Kwa upande mwingine, tunataka Serikali inunue mahindi yetu kwa bei ya Kshs2,200 kwa gunia. Serikali ikifanya hivyo, itakuwa heri kwa watu wetu ingawa wanaoishi mijini wataumia. Jukumu kubwa la Serikali ni kuhakikisha kuwepo kwa usawa katika pande zote. Tunataka Serikali iwashughulikie ipasavyo wakulima wa nafaka na wanunuzi. Ningependa kuwaeleza waheshimiwa Wabunge kwamba kwa miaka mingi, Serikali yetu haijashughulikia kilimo ipasavyo. Pesa ambazo zinatengewa Wizara ya Kilimo hazitoshi. Hata kiasi cha pesa kinachotengewa shirika la kutoa mikopo kwa wakulima, AFC, ambalo wakulima wengi hulitegemea, ni kidogo sana. Hata hivyo, mikakati ya hivi punde ya Serikali imewatia motisha wakulima. Mwaka uliopita, bei ya mahindi ilikuwa Kshs1,300 kwa gunia. Mwaka huu, gunia moja la mahindi linanunuliwa kwa Kshs1,700. Lakini changamoto kwa Wizara ni kwamba mkulima angependa bei hiyo iongezwe. Mnapotueleza kwamba bei ya mahindi itaongezwa, mtu ambaye yuko kule vijijini atalalamika hadi tuachwe vinywa wazi. Wakati Wakenya ambao wanaishi katika miji wanasema kwamba watafanya maandamano kupinga nyongezo ya bei ya unga, wakulima pia wanataka kufanya maandamano kushinikiza Serikali iongeze bei ya mahindi. Hii ni kwa sababu wakulima wameumia. Gharama ya upanzi imepanda. Haya ni mambo ambayo lazima tuyafahamu kama waheshimiwa Wabunge. Tunapozungumzia juu ya mikakati inayowekwa na Serikali, waheshimiwa Wabunge wengine wanalalamika kwamba hatua za Serikali haziwafikii. Serikali ikiitisha mkutano katika sehemu zao, wao hupuuza na kuleta siasa ndani ya masuala ya ukulima. Kwa hivyo, tushirikiane bega kwa bega mithili ya mchwa na nyuki ili tutatue jange la njaa katika taifa hili. Tatizo letu kubwa ni kwamba Serikali--- Tafadhali muagize mbolea ili gharama---"
}