GET /api/v0.1/hansard/entries/178557/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 178557,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/178557/?format=api",
    "text_counter": 317,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Ahsante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Hata kama dawa ni chungu, lakini itakuponya ugonjwa ulionao. Ningependa sote tushirikiane. Sharti tufahamu kwamba janga la njaa katika taifa la Kenya ni tisho kubwa. Kuna wale ambao wanataka nafaka yao inunuliwe kwa bei nzuri na kuna wale wanaolalamika eti bei ya unga imepanda. Pande hizi zote mbili zinahitaji kukaa November 26, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 3645 pamoja na Serikali izungumze nao. Ukweli ni kwamba kulikuwepo na tatizo la ukosefu wa mvua mwaka huo. Pia, tulikuwa na vita vya kisiasa ambavyo vimechangia kupunguka kwa uzalishaji. Ni lazima tuyazungumzie mambo haya kama viongozi. Sisi tunaotoka katika sehemu zinazozalisha nafaka, kwa sasa tumetulia huku tukingoja Serikali ichukue hatua. Lakini ninafikiri uvumilivu wetu utakapoisha, tutafanya maandamano kushinikiza Serikali iongeze bei ya kununua mahindi kutoka kwa wakulima. Naiomba Serikali ianze mipango ya kuagiza mbolea. Hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama ya kukuza nafaka. Tunataka tujue bei ya mbolea mapema ili wakulima nao waanze kujiandaa. Kwa hayo machache, ningependa kukushukuru, Bw. Naibu Spika wa Muda. Ikiwa kuna walaghai walioingia katika Halmashauri ya Nafaka (NCPB), basi tupewe majina yao. Hali ya kupakana matope haitatusaidia kama taifa. Tutafute ukweli."
}