GET /api/v0.1/hansard/entries/180339/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 180339,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/180339/?format=api",
"text_counter": 218,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mungatana",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Medical Services",
"speaker": {
"id": 185,
"legal_name": "Danson Buya Mungatana",
"slug": "danson-mungatana"
},
"content": " Bwana Naibu Spika wa Muda, ningependa kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa kunipa nafasi pia mimi nichangie Mswada huu, kuhusu sheria ya kutoza ushuru. Bwana Naibu Spika wa Muda, kwanza ningependa kumpongeza Waziri ambaye anashikilia Wizara ya Fedha kwa sasa. Mapendekezo ya Mswada huu ni ya maana sana, haswa tukiwafikiria ndugu na dada zetu ambao ni wananchi wa Kenya wa kawaida. Ningependa kuanza kwa kuzungumza kwa ujumla, na kulaumu kidogo. Bajeti iliposomwa mwezi wa sita, wananchi wengi walitarajia kwamba senti ambazo tumepitisha kwa Wizara kadha wa kadha zitawafikia mashinani na kazi itaanza kufanyika. Watu waliamini kwamba tulipitisha Bajeti iliyotokana na ushuru uliolipwa na wananchi. Lakini mwishoni mwa wiki iliyopita, tumefika nyumbani na kuzungumza na wananchi katika vikao. Najua kuwa Wabunge wenzangu wengine wamekaa katika vikao vya District Roads Committees (DRCs). Bwana Naibu Spika wa Muda, watu wameambiwa katika magazeti, maredio na katika matelevisheni kwamba kila eneo la ubunge limepewa Kshs17 milioni kusimamia barabara mwaka huu. Tuliporudi mashinani, na sote tukienda huko, wananchi wetu wanatuuliza katika mikutano hii: \"Senti hizi, mbona mvua inanyesha, barabara hii imeharibika na haijatengenezwa? Kwa nini barabara hii haijatengenezwa? Kwa nini barabara hii haijarekebishwa? Sisi tumeambiwa kuwa Wabunge wamepewa Kshs17 milioni katika kila eneo la ubunge kusimamia mambo ya urekebishaji wa barabara katika maeneo ya ubunge?\" Bwana Naibu Spika wa Muda, katika kupitisha Mswada huu, tunamuomba Waziri wa Muda wa Fedha, tafadhali, tukipitisha Bajeti yetu na watu wa Kenya Revenue Authority (KRA) wanatangaza katika maredio kuwa tumepitisha senti hizo, tafadhali wahakikishe kuwa senti hizo ziko katika maeneo yetu ya ubunge kwa wakati unaofaa! Haina maana sisi kupitisha hapa, halafu tukifika kule, tunaambiwa kuwa hatufanyi kazi! Kwa mfano, mpaka sasa, katika eneo langu la Ubunge la Garsen, tumepata Kshs5 milioni pekee yake kati ya Kshs17 milioni. Barabara ambazo tumeweza kutengeneza hadi sasa ni mbili tu na wananchi wanasikia katika redio kwamba pesa hizi zimetoka! Bwana Naibu Spika wa Muda, tungependa kumuomba Waziri ahakikishe kwamba tukiwa tumepitisha mipangilio hii na sheria hii, pesa hizi zifike mashinani haraka iwezekanavyo! Bwana Naibu Spika wa Muda, jambo la pili ambalo tungependa kusema leo ni kwamba tunamshukuru Waziri wa Muda wa Fedha kwa mipangilio yake ya kuhakikisha kwamba kuna"
}