HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 180341,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/180341/?format=api",
"text_counter": 220,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mungatana",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Medical Services",
"speaker": {
"id": 185,
"legal_name": "Danson Buya Mungatana",
"slug": "danson-mungatana"
},
"content": "ya Value Added Tax (VAT) kwa mkate na mchele. Lakini sisi tunawajua wafanya biashara wetu. Tunapitisha sheria hizi hapa, Waziri anakuja na Hoja hii vizuri na tunaipitisha, lakini hawapeleki faida hiyo kwa wananchi wa kawaida. Tungependa Waziri wa Muda wa Fedha alifikirie vizuri jambo hili. Ni mambo gani ambayo tungepitisha hapa Bungeni ili tukiwa tumekata ushuru kwa wale wanaoleta vyombo, ushuru huo au faida hiyo iwafikie wananchi? Ndio tunasema, kama Bunge, nikimuunga mkono mwenzangu Dr. Khalwale, ni lazima tuanze kufikiria namna kusimamia senti ambazo wananchi wanalipa kwa vyombo ambavyo wananunua. Hiyo ni lazima kwa sababu tutapitisha kuondoa ushuru kwa mikate leo, lakini kesho, tutalipa senti zile zile! November 11, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 3357 Anayefaidika ni mfanya biashara na sio mwananchi wa kawaida. Kwa hivyo, Waziri, lazima tufikirie zaidi jambo hili. Bwana Naibu Spika wa Muda, ukiangalia wasafiri wa ndege ambao wanatumia Kenya Airways--- Kila siku, tunapopata wawekezaji wengine ambao wanaingia katika biashara hiyo, unakuta nauli unayolipa kwenda Mombasa, Lamu au Malindi inashuka chini mara moja! Siku ambayo hao wengine wamefilisika au wamepata taabu yoyote, unaona bei inapanda tena. Tunakubali kuwa tuna zero rate usafiri wa kimataifa na tutaiunga mkono Kenya Airways. Lakini swali ni: Bei hizi za nauli za ndege zitashuka leo ama ni kitu tu tunawafanyia wao ili kuwaongezea faida? Tungependa Waziri alifikirie jambo hili, kwamba tukipitisha mambo hapa, inafaa mwananchi wa kawaida pia naye apate faida hiyo. Itakuwa ni jambo la kuhuzunisha sana kwamba sisi tunapitisha mambo hapa tukifikiria tunasaidia wananchi, kumbe anayefaidika ni kampuni, mwekaji rasilimali peke yake. Kwa hivyo, ni lazima Waziri jambo hili tulifikirie kwa urefu zaidi. Ni nini tutafanya ili tukipitisha jambo hapa Bungeni, mwananchi wa kawaida alipate? Kwa hivyo, tunaunga mkono jambo hilo, lakini je, mwananchi wa kawaida, faida hii ataipata lini? Bw. Naibu Spika wa Muda, vivyo hivyo Waziri alipotutangazia leo kuwa atashusha ushuru wa Import Duty kutoka asilimia 40 hadi asilimia 25 kwa simiti, watu wengi tunafanya kazi; sisi kama Wabunge tunajenga mashule na hospitali kupitia CDF. Je, Waziri atafanya namna gani faida hii itoke kwa wafanyibiashara peke yake, na iwafikie wananchi? Tungependa sana tulijibu swali hili kwa kirefu sana. Tunamshukuru Waziri na tunaunga mkono mipangilio ambayo iko katika Hoja hii kwa sababu kati ya mambo ambayo amependekeza kubadilisha kupitia kwa sheria hii ni Insurance Act. Kuna swala ambalo limetatiza wananchi siku nyingi sana. Watu wanaenda kortini baada ya kuumia katika ajali za barabarani au kazini na wanapewa fidia. Fidia ikilipwa, wakati wa korti kutoa zile pesa, unakuta kampuni za bima zinabaki na hizo pesa kwa muda mrefu. Wazo hili, ambalo limewekwa sasa la kubadilisha sheria ili kwamba kama hawatalipa pesa zilizoamuriwa na korti kwa muda wa siku 90, lazima walipe penalties ni zuri sana. Tungependelea hii ifanyike haraka iwezekanavyo kwa sababu ni wananchi wengi sana ambao wanadhulumiwa na makampuni ya bima hapa Kenya. Tungependa mambo yaanze kubadilika katika sekta ya uwekaji bima nchini Kenya. Tunafurahi sana ya kwamba sasa katika sheria ya kusimamia mipango ya barabarani, Traffic Act, Waziri anasema kwamba gari zote sasa ambazo zitakuwa zikiletwa nchini, lazima kabla ya kuachiliwa na Idara ya Forodha ziwe zimepewa vibali, zile ambazo zitatumika hapa nchini. Si zile za kwenda nje! Jambo la magari kwa wananchi wa kawaida wanaonunua magari ya"
}