GET /api/v0.1/hansard/entries/180343/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 180343,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/180343/?format=api",
    "text_counter": 222,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mungatana",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Medical Services",
    "speaker": {
        "id": 185,
        "legal_name": "Danson Buya Mungatana",
        "slug": "danson-mungatana"
    },
    "content": "kutoka nchi za nje, limewasumbua. Sheria hii ambayo tunaibadilisha siku ya leo ni ya kuhakikisha kuwa gari linatoka likiwa na number plate, ili liweze kufanya kazi mara moja badala ya kumsumbua wananchi. Hili ni jambo zuri na la kufaa kwa wananchi wa kawaida. Tunajua kuwa hawana senti za kuchukua gari mpya kutoka kwa makampuni, na badala ya kusumbuliwa, inafaa warahisishiwe mambo. Kwa njia hii mwananchi wa kawaida anafaidika sana. Bw. Naibu Spika wa Muda, mambo haya ambayo tunataka kuyazungumza siku ya leo ni mazuri. Tunamwomba Waziri kuona kuwa tukiyapitisha hapa yanamfikia mwananchi wa kawaida; sisi tukifanya kazi yetu hapa, inafaa mwananchi wa kawaida naye anafaidike, na isiwe tu ni wale wafanyikazi na wawekezaji mali peke yake ndio wanaofaidika. Kwa hayo machache, nashukuru na ninaunga mkono Hoja hii."
}