GET /api/v0.1/hansard/entries/181608/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 181608,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/181608/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mungatana",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Medical Services",
    "speaker": {
        "id": 185,
        "legal_name": "Danson Buya Mungatana",
        "slug": "danson-mungatana"
    },
    "content": " Ahsante, Mheshimiwa Naibu wa Spika, kwa kunipa nafasi ili nichangie Hoja iliyo mbele yetu. Pili, namshukuru Dr. Eseli kwa kuleta Hoja hii mbele ya Bunge kuzungumzia maswala muhimu kuhusu mipangilio ya kugawanya mali katika nchi ya Kenya. Pia, namshukuru mhe. Kaino kwa kuunga mkono Hoja iliyoletwa na Dr. Eseli. Yangu hayatakuwa mazungumzo marefu. Nataka kusema kwanza kwamba nakubaliana kabisa na wenzangu wote ambao wameizungumzia Hoja hii kwa kirefu. Lakini, nataka pia kukosoa kidogo kwa kusema kwamba, pengine siyo mahali unakotoka ambako kumeleta shida ya ugawanyaji wa rasilmali katika Kenya. Siyo kwa sababu umetoka Nairobi ndio unapata rasilmali nyingi. Siyo kwamba umetoka Mkoa wa Kati ndio umepata nyingi. Ama umetoka Kisumu ndio unapata nyingi. Sababu kubwa ya taabu katika ugawanyaji wa rasimali hapa Kenya ni namna Serikali ilivyoundwa kwa sasa."
}