GET /api/v0.1/hansard/entries/181612/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 181612,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/181612/?format=api",
    "text_counter": 232,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mungatana",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Medical Services",
    "speaker": {
        "id": 185,
        "legal_name": "Danson Buya Mungatana",
        "slug": "danson-mungatana"
    },
    "content": "Mfumo was Serikali uliopo kwa sasa umeathiri maeneo ambayo yako kando kando na Jiji la Nairobi. Umeathiri maeneo ambayo hayana watu wengi. Kenya hii, tukubali au tusikubali, tuko na mikoa minane. Kuna sehemu ambazo Mwenyezi Mungu amezipatia fanaka. Amezipatia mvua nyingi na watu ni wengi. Kuna sehemu ambazo zina watu wachache. Ukichukulia mfano wa Kisii na Garsen, kuna fanaka huko na kwingine hakuna. Mvua inachukua muda mrefu kunyesha. Ukilinganisha Garsen na Kirinyaga, kuna fanaka sehemu hiyo. Lakini sehemu nyingine hakuna kwa sababu ya mvua. Wananchi wanaishi kwa taabu. Lakini mpangilio wa Serikali ambayo tuko nao tangu Uhuru, ndio unaleta matata. Taabu ilioko ni kwamba, sisi katika Bunge, hasa Bunge hili la Kumi, tumezungumza na kusema kwamba kuna umuhimu wa swala la ugawaji wa rasilmali hapa Kenya uangaliwe kwa undani. Lakini, hata tukipitisha Hoja hii - na tumepitisha nyingi - utakuta kwamba ndani ya Serikali, kuna mipangalio ya kiserikali. Inakuwa kwamba mazungumzo ya Bunge hayatekelezwi katika Wizara mbali mbali. Hii ndio taabu ilioko. Swali ambalo tungependa kuliuliza ni: \"Je, Bunge ni mjakazi wa Serikali ya nje ama Serikali ni mjakazi wa Bunge?\" Inayokuja kwanza ni Serikali ama ni Bunge? Nani alimzaa nani? Hayo ndio maswali ambayo ni lazima tujiulize. Katika mawazo yangu, najua kwamba Bunge ndio mama mzazi wa Serikali. Lakini kwa sasa ukiangalia, ni kana kwamba Bunge limekuwa mjakazi wa Serikali. Hivi sasa, tukipitisha Hoja hii na kusema kwamba ni lazima tuwe na usawa katika ugavi wa rasilmali ya Kenya, kuna watu katika Serikali, katika Utumishi wa Umma, watasema hayo ni mazungumzo ya Bunge. Wacha yaishie pale Bunge. Hiyo ni kwa sababu wanajua mfumo wa Serikali. Wao ndio wanapanga Bajeti na sisi tunakuja kupitisha. Ningependa ndugu zangu waheshimiwa, wakati huu ambapo tunataka kubadilisha hii Katiba, tuhakikishe ya kwamba Serikali itakuwa mjakazi wa hii Bunge. Tukipitisha maneno hapa, yataenda kutekelezwa na Serikali kuu. Jambo mmoja ambalo ni lazima tupitishe ni kwamba kutoka kitengo cha Katibu wa Kudumu kushuka chini - watumishi wakuu wa Serikali kama vile wakurugenzi - wawe wanaajiriwa kwa mkataba. Wasiwe wafanyakazi wa Serikali haswa. Wawe watu waliopewa mkataba. Huko Marekani, wafanyakazi wa kitengo cha juu wanajua kabisa Serikali ya George Bush ikiisha, wanatoa barua ya kuwacha kazi. Kwa sababu gani? Kwa sababu Rais mpya atakayekuja atakuja na maswala yake na mipangilio yake. Yule wa kuhakikisha inatekelezwa ni yule ambaye yuko kule ndani. Ikiwa ni wale wale ndio watatupangia--- Ni wale wale ambao watatupangia mwaka kesho na mwaka ujao, inakuwa ni kazi ngumu kwa Bunge hili kuwatumikia wananchi inavyopaswa. Kwa hivyo, ningewaomba wenzangu Wabunge kwamba, wakati huu, tuko na nafasi. Wakati tutakapobadilisha Katiba yetu, tuhakikishe ya kwamba sisi Wabunge tumejipatia mamlaka ya kutosha kuhakikisha kwamba maneno tunayoyazungumza hapa yanatekelezwa na Serikali. Tukifanya hivyo, tutarejesha heshima na nafasi ya Bunge katika Kenya. Tumekuwa na taabu. Mazungumzo tunayafanya hapa. Tunaleta mambo kutoka kwa waliotuchagua. Tunayazungumza hapa na kupitisha. Lakini kutekelezwa inakuwa ni taabu kubwa. Kwa hivyo, ningependa kuunga mkono Hoja hii kwa nguvu sana. Lakini nasema ya kwamba, pamoja na mazungumzo tutakayoyafanya hapa, tuhakikishe ya kwamba wakati tunaleta mazungumuzo ya kubadilisha Katiba, sisi Wabunge wa Bunge la Kenya tumechukua mamlaka ili kuhakikisha wananchi wanapata haki yao. Kwa hayo mengi, naunga mkono Hoja hii. 3094 PARLIAMENTARY DEBATE October 29, 2008"
}