HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 181618,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/181618/?format=api",
"text_counter": 238,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, nasimama hapa kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Dk. Eseli. Ni jambo la uwazi kuwa ugawaji wa raslimali katika nchi hii umeelekezwa mahali fulani. Hata mtoto mchanga analiona hilo jambo. Kwa hivyo, tunaomba kwamba wakati huu madhumuni yetu ni kuangalia kuwa yale ambayo yalikuwa yametendeka kuhusu ugawaji wa raslimali--- Siko hapa kusema kwamba umeenda mahali fulani, lakini ugawaji wa raslimali ya nchi hii utegemee, kwanza, watu walio mahali fulani. Jambo la pili ni kwamba utegemee eneo ambalo linahusika katika ugawaji wa raslimali. Naomba nikupatie mfano; katika Mkoa wa Pwani. Kodi ambayo inatoka bandarini ndiyo kodi kubwa zaidi katika mikoa yetu nchini. Lakini angalia ugawaji! Wakati hiyo kodi imeingia katika Serikali kuu inagawanywa namna gani? Angalia ndugu zetu ambao wako Likoni; huwezi kuamini kwamba wale watu ndiyo wanaishi 3096 PARLIAMENTARY DEBATE October 29, 2008 karibu na bandari. Hiyo kodi inaenda wapi? Ikiwa ni ugawanyaji inapelekwa wapi na wale wanaofaidika na hiyo raslimali ni kina nani? Bw. Naibu Spika wa Muda, nikirudi katika sehemu ambayo ninawakilisha ya Wundanyi, Taita, utakuta kwamba barabara zetu ni haba, maji hamna, shule hamna, na si kuwa hatuna raslimali. Zipo! Lakini zinaenda wapi? Maji ambayo yananywewa Mombasa yanatoka Milima Taita. Wakati ule yalikuwa yanashughulikiwa na National Water Conservation and Pipeline Corporation, wakikusanya zile fedha walikuwa hawazirudishi kwa mfereji, ama kwa bomba, ili kurekebisha lile bomba na kuzileta kwa Serikali kuu, ndipo zigawanywe. Ni pahali pamoja peke yake nimeona watu wanatoa mchango wa mali ile walio nayo iuzwe, na yule ambaye anaichukua anaichukua bure, na akipata zile hela yeye anaamua atazitumia aje, na wala hafikirii mahali ile mali imetoka. Hii ndiyo sababu tunasema kwamba National Water Conservation and Pipeline Corporation ilikuwa imewajibika kuhakikisha kuwa mfereji wa Mzima Springs umerekebishwa na maji mengine yamegawiwa watu wa Taita, huku maji mengine yakienda Mombasa. Kodi kutokana na maji haikufaa kwenda kwa Serikali kuu na kugawiwa mahali kwingine, na huku wale ambao wametoa hayo maji hawakupatiwa chochote. Tunaona kwamba kulikuwa na njama ya kuhakikisha kuwa ugawaji wa raslimali katika nchi hii umeelekezwa mahali fulani. Nikisema hivi ninamaanisha nini? Angalia mbuga za wanyama kama Tsavo East na Tsavo West, kuna wanyama kadhaa wa kadhaa. Wakenya wenyewe wanakubaliana na mimi kuwa zile hela ambazo zinaingia nchini kutokana na watalii wanaoenda kutalii Tsavo East na Tsavo West zinaweza kujenga barabara nyingi zikitumiwa vizuri. Wale watu ambao wanapakana na mbuga hizi wanapata nini? Hela zote zinakusanywa, zinaingia katika mfuko wa serikali na kupelekwa kwingine. Hakuna mtu ambaye anaweza kuniambia hapa kuwa Serikali imeanza kulinda wanyama tangu hapo awali. Tangu hapo, wanyama walikuwa wanalindwa na wenyeji. Serikali imekuta wanyama wamelindwa na wenyeji na ikawachukua wanyama hawa kuwa wake. Tumekubali wanyama hawa ni wa Serikali lakini yale mapato yanayopatikana kutokana na watalii ambao wameingia hapa nchini yanamfaidi nani? Bw. Naibu Spika wa Muda, hii ndiyo sababu tumeleta Hoja hii ili tuangalie jinsi rasilmali zinaweza kugawanywa kwa uhaki. Yule ndovu aliye Maasai Mara ni sawa na ndovu ambaye yuko katika Mbuga ya Tsavo National. Utakuta watoto ambao wanakuwa katika mtaa wa Maasai Mara wanasomeshwa na hela ambazo zinatokana na watalii. Lakini watoto Wataita hawasomeshwi. Tunasema huo si usawa. Ugawaji wa rasilmali zetu umeenda upande mmoja. Tunaomba madhambi haya yarekebishwe. Tukiangalia madini, inasemekana kwamba asilimia themanini ya rasilmali ya nchi hii iko Mkoa wa Pwani. Tuna Coffee Board, Tea Board na Lake Basin Development Authority. Ni shirika gani limeundwa na Serikali kuangalia kwamba madini katika Mkoa wa Pwani yanatumiwa kisawa na kuwa wenyeji na Serikali wanafaidika? Tukiangalia Mkoa wa Kaskazini Mashariki, watu wale wanafuga ng'ombe. Lakini tumefanya nini kuhakikisha kuwa ng'ombe wao wanauzwa vizuri; wamepata kichinjio karibu na kupata mauzo? Itambidi mtu atoke North Eastern na ng'ombe awasafirishe mpaka hapa Athi River waje kuchinjwa. Je, hiki kichinjio kingekuwa kimepelekwa kule juu, si watu wale wangefaidika? Serikali ihakikishe kuwa rasilmali zinagawanywa vile zinavyostahili ili kila mtu ambaye anaishi nchini humu aone anafaidika kwa zile rasilmali za nchi. Ni jambo la kusikitisha kuwa mkoa mzima unawapeleka wanafunzi 12 katika chuo kikuu na ilhali shule moja katika sehemu zingine hapa nchini inawachukua wanafunzi 200 ama 300 katika chuo kikuu. Mtihani wanaofanya ni ule ule mmoja. Ukiangalia shule hizo ambazo hawa watoto wanafunzwa hazina vifaa na mtihani ni mmoja. Je, kuna usawa hapo? Kweli tunahitaji mtu awe profesa wa taaluma ya hesabu ya fedha ajue kuwa hamna usawa wa ugawaji wa rasilmali nchini humu? Utakuta mikoa mingine ina shule, barabara na kila kitu na mingine haina chochote. October 29, 2008 PARLIAMENTARY DEBATES 3097 Jana tulienda kuwaangalia watoto wale mapacha ambao walizaliwa wakiwa wameshikamana. Imebidi watolewe Mombasa waletwe mpaka Kenyatta National Hospital na hii si mara ya kwanza. Je, hizi hospitali zetu kubwa kubwa zingekuwa zimepatiwa vifaa vya kutosha na kupanuliwa, hakungekuwa na haja ya watoto hawa kutolewa Mombasa na kuletwa hapa Nairobi. Tunaona kuwa rasilmali za nchi zimewekwa mahali pamoja na huku wengine wamekosa kabisa. Akina mama ambao walikuwa vijijini katika mikoa mbali mbali wanaweza kufa hasa wakati wa kujifungua kwa sababu hakuna vifaa katika hospitali. Ukiuliza kwa sababu gani, utakuta kuwa kila hela zinazochukuliwa zinaletwa Nairobi. Mfano ni ugawaji wa hela za maji mwaka jana. Hii ndio maana ninaomba niwakosoe wale ambao wanasema kuwa labda kuna mawazo duni kuwa hela nyingi zimepelekwa Mkoa wa Kati. Si mawazo duni. Ni mambo tumeona yakitendeka tangu tuwe vijana na hivi sasa sisi ni waheshimiwa Wabunge. Itakuwa ni jambo la aibu sisi kama waheshimiwa Wabunge tukiona mambo kama haya yakitendeka na tunanyamaza. Wakati umefika tuambiane ukweli na tuseme rasilmali zigawanywe kwa haki. Rasilmali zinafaa zigawanywe kulingana na hali ilivyo lakini zote zisirundukwe mahali pamoja kwa sababu mtu fulani ni Waziri. Ukiwa Waziri, basi, hela zitapelekwa kwako. Ukiwa Waziri wa Maji basi hela za maji itapelekwa kwako. Ukiwa Waziri wa Uchumi, hela za uchumi zitapelekwa kwako. Ukiwa Waziri wa Barabara basi barabara zako zitatengenezwa. Tunasema la! Tunataka tuwe na usawa nchini na tuhakikishe kwamba kila mwananchi anapata haki yake. Tukiendelea kunyamaza na dhambi kama hii inatendeka, tutajikuta tuko pale pale ambapo tumetoka mapema mwaka huu, kwa maoni yangu. Kitu kilichowafanya watu wakazozana, kuraruliana nguo na kupigana kwa mishale na silaha zingine ni kwa sababu ya rasilmali. Watu wengi walikuwa na uchungu. Wengi wamenyang'anywa mali yao. Watu wametoka huku juu bara wakaenda Pwani wakaona mashamba hayo hayana wenyewe; wameyavamia. Wanatoka Nairobi na vyeti vya umilikaji shamba na kukuambia: \"Ondoka, nenda, nina title deed; wewe huna.\" Kwa nini Serikali isitoe pesa ihakikishe kuwa watu hawa wamepewa stakabadhi za kumiliki mashamba? Tunanyamaza tu. Na watu wanasema tuendelee vivyo hivyo. Tunasema la! Haitaendelea hivyo hivyo na hatutaruhusu mambo kama haya yaendelee. Uonevu huu umepitwa na wakati. Tunatakiwa kutambua kuwa sisi wote ni Wakenya na tuna haki ya kuishi nchini humu na haki ya rasilmali zetu za nchi hii. Kwa hayo machache, naomba niunge mkono Hoja hii. Asante."
}