GET /api/v0.1/hansard/entries/181619/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 181619,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/181619/?format=api",
"text_counter": 239,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Twaha",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 145,
"legal_name": "Yasin Fahim Twaha",
"slug": "yasin-twaha"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii nami nichangie Hoja hii. Ningependa kuwapongeza waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Tisa wakiongozwa na Eng. Karue aliyekuwa Mbunge wa Ol Kalou kwa kuleta Hoja ya CDF na tukaipitisha. Mimi nilikuwa mmoja wa Wabunge hao waliopitisha Hoja hiyo. Kwa sasa, kuna usawa katika Kenya kuliko vile ilivyokuwa. Kama vile Dr. Eseli alivyopendekeza, kuna haja ya kurekebisha mambo fulani. CDF imetuwezesha kujenga shule za msingi na za upili katika kila lokesheni. Tumesambaza maji katika sehemu ambazo maji hayakuwa. Tumejenga zahanati na vile vile, tumewasaidia wananchi kwa njia nyingi kutumia pesa za CDF. Kwa hivyo, tunashukuru Mungu kwa sababu pesa za CDF zipo. Sasa tunatakikana kuboresha maadili ya ugawanyaji wa pesa za CDF. Ninaunga mkono Hoja ya Dr. Eseli kwamba kuna haja ya kuyarekebisha mambo. Nitatoa mfano. Kule kwangu, Lamu Magharibi, nina wapigaji kura 31,000. Jirani yangu huko Lamu Mashariki ana wapigaji kura 11,000. Huko Lamu Mashariki wanapata Kshs36 million. Lamu Magharibi ambayo ina wapigaji kura 20,000 zaidi inapata Kshs41 million. Yaani zile Kshs5 milioni za ziada zinawahudumia watu 20,000 zaidi ya wale wengine. Ninapata maswali magumu kwa sababu sisi ni majirani. Ninaulizwa mbona kule wanafunzi wanalipiwa karo ya shule yote na 3098 PARLIAMENTARY DEBATE October 29, 2008 sisi tunalipiwa kidogo. Jawabu ni kwamba kule kuna watu wachache na sisi tuna watu wengi na pesa ni karibu sawa sawa. Kwa hivyo, ni muhimu tuunge mkono hii Hoja ya Dr. Eseli ili mambo kama idadi ya watu yaangaliwe wakati wa kugawa pesa hizi. Kabla hatujafika hapo lazima kuwa na kongamano. Tunafaa tukubaliane vizuri tujue mabadiliko haya yatakuwa namna gani. Mabadiliko hayafai kuwa mabaya kuliko vile tuko sasa. Kuna maonevu katika kugawana rasilmali. Ukiangalia Mkoa wa Pwani kuna wilaya nane. Nafikiri juzi Tana River wameongeza zingine, zimekuwa tisa. Wilaya pekee ambaye haina bara bara ya lami ni Lamu kwa miaka 45 kutoka tupate Uhuru. Mahali ambapo lami imemalizika ni kutoka Garsen kuingia Lamu District. Kwa hivyo, ni lazima mambo haya yaangaliwe. Tunashukuru Serikali ya Rais Kibaki kwa kufanya planning na design. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuna mimea ambayo sisi tunakuza kama vile korosho na bixa. Tulipopata soko huru katika Kenya, uuzaji wa mimea yote ukawa katika soko huru. Lakini bixa na korosho ziliorodheshwa kama scheduled crops ambayo sijui maana yake. Nimesoma Kiingereza, lakini orodha hii inamaanisha kuwa ni lazima umuuzie ule mnunuzi mmoja kwa bei anayoitaka. Werevu ukizidi unakuwa ujinga. Wakaweka bei chini sana mpaka watu wakakosa kuuza hiyo mimea na mtambo ukafungwa kwa kukosa mazao. Hii ni dhuluma ambayo ilitokea. Sasa kumetokea dhuluma nyingine. Waziri wa Kilimo ameweka kodi kwa watu ambao wanasafirisha korosho au bixa mbichi. Ni lazima hawa watu walipe kodi ya asilimia ishirini. Anadai kwamba kodi hii itasaidia kukuza viwanda. Kwa bahati mbaya au nzuri, hawa wanunuzi wananunua na kusafirisha bixa ikiwa mbichi, lakini ile gharama ya kodi, wanaisukumia mkulima. Kama walikuwa wakinunua kwa Kshs20 kwa mkulima, sasa watanunua kwa Kshs16 ili yule mkulima alipe ule ushuru. Yule mkulima ni maskini na hana njia ya kufika sokoni na inambidi auze mazao yake kwa bei ya chini. Ningeomba Serikali iondoe huo ushuru wa korosho ili wakulima wanufaike. Korosho ndiyo inalipia watoto karo ya shule na mambo mengine. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}